Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na
Askari wa Jeshi la Polisi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Kikuu cha Polisi
(Central) wakati alipokitembelea kituo hicho cha Polisi jijini Dar es Salaam
leo. Pia Waziri Kitwanga katika ziara yake hiyo ya kwanza tangu alipoteuliwa
kuiongoza wizara hiyo, alitembelea Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
(DPA), pamoja na kukagua nyumba za Makazi ya Polisi za sasa na zamani zilizopo
barabara ya Kilwa. Wanne kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akitoka kuikagua moja ya
nyumba ya zamani ya Jeshi ya Polisi ambayo inakaliwa na baadhi ya askari
iliyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Mbarak Abdulwakil. Waziri Kitwanga alizikagua nyumba hizo za zamani
pamoja na zakisasa zilizopo katika eneo hilo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiiangalia nyumba ya
mabati ya makazi ya Polisi wakati alipoingia ndani huku akitokwa na jasho kutokana
na joto kali ndani ya nyumba hiyo. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kutembelea
nyumba hizo zilizopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na kushoto
ni mkazi wa nyumba hiyo, ambaye ni
askari Polisi, Nelson Chale.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kushoto) wakizikagua nyumba za kisasa ambazo ni
za ghorofa za Jeshi ya Polisi nchini zilizopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es
Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara kuzitembelea nyumba hizo ili kujionea
ukosefu wa nyumba unaowakabili Polisi nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai), Mkuu wa Utawala wa Jeshi
la Polisi, Kamishina Thobias Andengenye (kulia) na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya
Polisi Dar es Salaam (DPA), DCP Ally Lugendo (wapili kulia) wakikwepa waya
wakati walipokuwa wanamuonyesha Waziri Kitwanga mabweni ya Chuo hicho kilichopo
barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akilikagua moja ya darasa
linalotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA).
Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kukitembelea chuo hicho pamoja na kuzungumza
na wakufunzi wa chuo hicho.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akionyeshwa moja ya gari
la maji washa, na Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman
Kova katika Kambi ya Jeshi la Polisi iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es
Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya
Jeshi hilo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), akiwauliza maswali Mkuu
wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Kamishina Thobias Andengenye (kushoto) na Mkuu
wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), DCP Ally Lugendo wakati
Waziri huyo alipofanya ziara katika Chuo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa,
jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara hiyo ili ajifunze mambo
mbalimbali yanayofanywa na Jeshi la Polisi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), akimsikiliza kwa makini
Mkufunzi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), Inspekta Novatus
Akondowe (kulia) alipokuwa anamuuliza swali. Waziri Kitwanga alitoa ruhusa ya
kila mkufunzi wa chuo hilo waeleze matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo
chuoni hapo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akijibu maswali mbalimbali ya
waandishi wa habari alioambatana nao wakati wa ziara yake katika Chuo cha
Taaluma ya Polisi kilichopo jijini Dar es Salaam. Pia Waziri huyo katika ziara
yake hiyo ya kwanza tangu alipoteuliwa kuiongoza Wizara hiyo, alitembelea
nyumba ya Makazi ya Polisi barabara ya Kilwa, Kituo Kikuu cha Polisi (Central),
Kituo cha Polisi Msimbazi na Kituo cha Polisi Oysterbay. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
No comments:
Post a Comment