Thursday, December 17, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Inaelezwa kuwa takribani kaya 8543 kati ya 9000 hazina vyoo wilayani Chato mkoani Geita; https://youtu.be/m31tZxLsJB0

Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mchungaji mmoja kwa kosa la ukatili wa kijinsia baada ya kumfunga kamba mtoto wao na kisha kumfungia ndani ya nyumba; https://youtu.be/dBzwwS5YtkI

Umoja wa wakuu wa shule za sekondari TAHOSSA nchini umeitaka serikali kupeleka pesa za kuendeshea shule kwa wakati;https://youtu.be/Xk8mPmRfNw0

Inaelezwa kuwa sekta ya kilimo cha matunda,mbogamboga pamoja na maua imekua na mchango mkubwa katika kuliingizia taifa pato;https://youtu.be/smV0NSeEc-8

Makocha nchini wameshauriwa kufanya juhudi katika kuibua vipaji vya walinda milango nchini; https://youtu.be/K368omqXeEw

Mtuhumiwa wa kesi ya rushwa ndani ya shirikisho la mpira wa miguu duniani Eduardo Li, amekubali shauri lake lipelekwe nchini Marekani; https://youtu.be/tIir0N612eo  

Rais Magufuli atengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU kufuatia kushindwa kudhibiti rushwa na utoroshwaji makontena.https://youtu.be/DlbTiy8NcO4

Walimu kutoka mikoa 3 ya Tanzania bara wafaidika na mafunzo ya kuboresha taaluma katika shule zao kuendana na matokeo makubwa sasa. https://youtu.be/SATmFelGYnc   

Mgambo wa halmashauri ya manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam wanusurika kipigo katika eneo la feri kabla ya kuokolewa na askari wanaolinda katika ofisi ya waziri mkuu. https://youtu.be/gP-ZSdUsjXU  

Japan imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za uchumi, manedeleo na ushirikiano wa kimataifa kufuatia ujumbe wa waziri mkuu wa nchi hiyo hapa nchini.https://youtu.be/mbljxCkFby0  

Waziri wa kazi, ajira, vijana na walemavu Jenister Mhagama aagiza kusitishwa kwa ujenzi wa mtaro wa maji taka eneo la Buguruni kufuatia kujengwa chini ya kiwango.https://youtu.be/mNyWWnrvzeg   

Mamenenja wa kanda wa Tanesco waambiwa kujiandaa kuachia ngazi zao endapo hawatashughulikia kwa haraka kero za umeme zinazowakumba wateja katika maeneo yao.https://youtu.be/O0XOyVaFu1U

Waziri wa mambo ya ndani Mhe.Charles Kitwanga asema jeshi la polisi litawachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika kwenye mgogoro baina ya wafugaji na wakulima wilayani Mvomero.https://youtu.be/2TQhhWPpEAY  
  

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA yaingia lawamani baada ya wafanyabiashara kuwatuhumu kuwanyanganya bidhaa zilizopo dukani bila ya kutoa taarifa yeyote. https://youtu.be/xmCgX4B3Ogc  

Mapigano mapya yaibuka katika wilaya ya Kilosa baada ya wakulima 11 kuvamiwa na kupigwa na wafugaji wakati wakielekea kuangalia mipaka ya mashamba yao. https://youtu.be/rBKdLFqtDug  

Serikali mkoani Kilimanjaro imetoa tahadhari kwa wakazi waishio maeneo yenye miinuko kuchukua tahadhari kutokana na athari zinazoendelea kusababishwa na mvua.https://youtu.be/o1471SBCCVY   

Habari zinasema Meli ya Mv. Royal Express iliyokuwa ikitoka Pemba kuelekea Unguja imepata hitilafu chumba cha injini na kupelekea mlipuko wa moto huku abiria wote wakiokolewa.https://youtu.be/gPKUW3daxBQ

Rais John Magufuli ametengua utezi wa mkurugenzi wa TAKUKURU kwa madai ya kutoridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa taasisi hiyo;https://youtu.be/2FvvCHE3zLA

Zaidi ya asasi 40 zinazofanya  kazi  na wafugaji asilia zimelaani vitendo vya uvunjifu wa amani unaofanywa baina ya wafugaji na wakulima nchini; https://youtu.be/-OAcAVfOWvk

Mfanyabiashara mmoja wa madini raia wa India amekamatwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA, akiwa na vipande 264 vya madini aina ya Tanzanite;https://youtu.be/CrsTzyekY2k

Wizara ya maji na umwagiliaji imepitisha mfumo wa mkataba wa kiutendaji katika kukabiliana na watumishi wazembe;https://youtu.be/hP08_dXh0SY

Benki ya Akiba imepanua wigo wa utoaji wa huduma zake za kibenki kwa kuanza kutoa huduma za bima kwa wateja wake;https://youtu.be/vR7pRCCFDMI

Benki ya NMB imezindua mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za wateja wake ili kurahishia wateja wake wanaoomba mikopo kuipata kwa haraka na kwa urahisi; https://youtu.be/Neu_QcP2WL8

Serikali imepitisha sheria itakayo vitaka vyombo vya habari hapa nchini kuwalipa wasanii kwa kila nyimbo watakazozicheza;https://youtu.be/GV9DN0b3hBk

No comments: