Thursday, December 17, 2015

WATANZANIA WANNE WAPATA TUZO ZA UANDISHI WA FASIHI YA KISWAHILI AFRIKA

Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani)jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi na Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah.
Mkuu wa Idara ya Fasihi ya Mawasiliano na Uchapishaji (TATAKI) WA wa chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwa na baadhi ya viongozi ya ALAF Limited. 
Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi akipokea ua kutoka kwa Meneja Huduma na Masooko Alaf ,Piyush Kanti Nath leo wakati wa kuwapongeza washindi wa uanishi wa fasihi za kiswahili Afrika.
Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na tuzo aliyoipata katika uandishi wa wa kitabu cha Kolonia ya Santita.
Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi.


Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

KWA mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika rekodi ya dunia kwa watanzania wanne kuchomoza katika tuzo ya waandishi ya Fasihi Afrika. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei amesema lugha ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania wenye lugha yao kuwa washindi.

Washindi wa tuzo hizo ni Enock Maregesi ambaye aliandika Kolonia Santita,Chiristophee Bubebah, Anna Manyaza aliandika Penzi la Damu, Mohamed Ghassani aliandika N’na Kwetu.

Walioshiriki katika tuzo hiyo walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni washindi wakitokea nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.

Amesema kwa lugha ya kifaransa na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka kwa watu kuandika riwaya na mashairi lakini Kiswahili imekuwa ikisahaulika hivyo na kufanya Chuo Cornell Nchini Marekani iliamua kufanya hivyo kuwa watu kuandika Riwaya na Mashairi.

Katika tuzo hizo Kampuni ya watengenezaji wa Mabati ya Alaf ilizamini tuzo hizo na kutaka watu wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.


Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na watanzania katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.

No comments: