Friday, December 18, 2015

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku moja wa baraza hilo unaofanyika katika Ukumbi wa Jeshi la Magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone. Katika kikao hicho Abdulwakil aliwataka watumishi wa wizara yake wafanye kazi kwa uadilifu na weledi ili kuleta mafanikio ndani ya wizara hiyo muhimu katika maendeleo ya nchi.
Katibu Mkuu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara hiyo, Obeid Mbaga. Wapili kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Amani Mashaka, anayefuata ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo, Jenita Ndone wakiwaongoza wajumbe wa Baraza hilo kuimba wimbo wa mshikamano daima kabla ya Katibu Mkuu kufungua kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Obeid Mbaga akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) kuja kuzungumza na wajumbe wa kikao hicho (hawapo pichani) kabla ya kufungua rasmi kikao hicho. Kushoto meza kuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mtoa Mada wa Benki ya NMB, Faraja Kaziulaya akiwasilisha mada ya jinsi wanavyotoa huduma zao pamoja na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo, wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (meza ya mbele kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo wakiwa na baadhi wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, wakimsikiliza kwa makini mtoa Mada wa Benki ya NMB, Faraja Kaziulaya (hayupo pichani) akiiwasilisha mada ya jinsi wanavyotoa huduma zao pamoja na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo. Abdulwakil alifungua kikao cha Baraza hilo na wajumbe walijadili masuala mbalimbali ya kuiendeleza Wizara hiyo zaidi.
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Zanzibar, Shemsa Said akichangia mada katika kikao cha Baraza hilo kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wanne kushoto waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Mngodo (watatu kushoto waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.

No comments: