Ikiwa ni
siku chache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Nchi
Wanachama COP21 uliokuwa ukifanyika Paris, Ufaransa, ambao ulimalizika kwa
kupitisha mkataba mpya wa mabadiliko ya tabianchi (Paris Agreement), wadau mbalimbali
wamekutana kujadili matokeo ya mkutano huo.
Mkutano huo wa
wadau umeandaliwa na ForumCC kwa kushirikiana na Rosa Luxemburg
Stiftung (RLS) kwa lengo la kuangalia mazidi na mapungufu ya mkataba huo ambao
umeweka historia mpya ya kuelekea juhudi za kupunguza ongezeko la joto duniani,
kukabiliana na kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Miongoni mwa vipengele vya mkataba huo vilivyojadiliwa na
wadau hao ni pamoja na Kiwango cha nyuzi joto, Upunguzaji wa gesi Joto, Kukabiliana na mabadiliko ya tabainchi,
Uharibifu na upotevu, Fedha za mabadiliko ya tabianchi, Mfumo wa taasisi na
ushiriki wa serikali, waandishi wa habari pamoja na asasi za kiraia kwenye
kuleta mchango wa makubaliano ya mkataba huo.
Picha ya pamoja ya Wadau hao
Mwakilishi
wa ForumCC, Adam Athony akitoa mrejesho wa kilichojiri kwenye Mkutano
wa Mbadailiko ya Tabianchi COP21 uliofanyika Paris, Ufaransa
Mwakilishi wa Rosa Luxemburg
Stiftung (RLS) Afrika Mashariki, Musa Bulegeya (katikati)
akizungumza jambo wakati wa mkutano huo, kulia kwake ni Meneja Miradi
ForumCC Rebecca Muna, wakati kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ForumCC
Yunista Kibona.
Mwandishi
wa habari na Mmiliki wa mtandao wa Tabianchi, Dotto Kahindi akitoa
mrejesho wa yale aliyojifunza kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi
COP21, Uliofanyika Paris, Ufaransa.
Washiriki wakifuatilia mkutano huo
Mwakilishi
wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ladslaus Kyaruzi akielezea namna
Tanzania ilivyoshiriki kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP21.
Picha zote na Jonathan Sawaya wa ForumCC
No comments:
Post a Comment