Wednesday, December 23, 2015

Profesa Mwansoko aandaa Mhadhara wa ukuzaji wa Kiswahili

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akifungua Mhadhara wa ukuzaji Kiswahili kupitia tafsiri ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko katika hafla ya kumuaga Mkurugenzi huyo anayemaliza muda wake wa utumishi wa umma.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akipokea rasimu ya awali ya ukuzaji wa Kiswahili kupitia Tafsiri ikiwa ni mchango wa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, anayekabidhi ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Dkt. Hadija Jilala.
Profesa Aladin Mutembei aliyesimama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichangia mada ya ukuza ji wa Kiswahili kupitia Tafsiri katika mhadhara ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko anayemaliza muda wake wa utumishi wa umma, kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko mara baada ya kufungua Mhadhara wa ukuzaji wa Kiswahili kutipia Tafsiri ulioandaliwa na Mkurugenzi huyo anayekaribia kumaliza muda wake wa Utumishi wa umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa za Maonesho (CHASAMATA) kulia na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kushoto Godrey Mwingereza mara baada ya mhadhara wa ukuzaji wa Kiswahili kutipia Tafsiri ulioandaliwa na Mkurugenzi huyo anayekaribia kumaliza muda wake wa Utumishi wa umma.
Katibu wa Bodi ya Filamu Joyce Fissoo akimpongeza Profesa Hermas Mwansoko mara baada ya mhadhara wa ukuzaji wa Kiswahili kutipia Tafsiri ulioandaliwa na Mkurugenzi huyo anayekaribia kumaliza muda wake wa Utumishi wa umma . (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM)

No comments: