Sunday, December 20, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Wakazi wa Mpanga Kipengele mkoani Mbeya wameilalamikia hifadhi ya Kipengele kwa madai ya vitendo vya unyanyasaji;https://youtu.be/9MgY_oOdwrU  

Serikali mkoani Manyara imetengua zoezi la kugawa maeneo kwa ajili ya ujenzi baada ya kubaini kuwepo kwa hali ya ufisadi; https://youtu.be/5brqBTb2uU4   

Baadhi ya wananchi mkoani Mbeya wameiomba serikali kuthibiti uuzaji wa mazao nje nchi ili kupambana na mfumko wa bei ya vyakula nchini;https://youtu.be/VcuhyuUALng  

Inaelezwa kuwa zikiwa zimebaki siku kadhaa kuelekea siku kuu za Krimasi na Mwaka mpya, bei ya bidhaa ya panda katika soko kuu jijini Mwanza;https://youtu.be/8VVEf2cQPoI  

Kocha mkuu wa timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza John Tegete amewataka viongozi wa timu hiyo kuwajali ikiwemo kuwapa haki zao;https://youtu.be/BBsQeThm0nk  

Rais wa zamani wa shirikisho soka la nchini Brazili , Marco Polo Del Nero amesema shutuma za rushwa anazopakaziwa si za kweli bali zinalenga kudhohofisha maendeleo ya soka nchini humo; https://youtu.be/HQTAxQatpgc 

Waziri wa maji na umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa afanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji mkoani Geita na kutoa maagizo mazito.https://youtu.be/a9LIgRYQtbo  

Taasisi ya mifupa ya MOI kwa kushirikiana na taasisi ya marafiki wa watoto wenye saratani Tanzania waendesha upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ili kunusuru maisha yao.https://youtu.be/RJMTIdNUl0I  

Waathirika waliokumbwa na bomoabomoa katika bonde la mto msimbazi waiomba serikali kuchunguza maafisa wa halimashauri za manispaa za jiji la Dar es salaam waliohusika kugawa viwanja katika eneo la Mabwepande.

Magogo 5876 yakamatwa na wakala wa misitu Tanzania katika maeneneo mbalimbali ya nyanda za juu kusini yakidhaniwa kuwa yametoka nchini Zambia.https://youtu.be/EWlNJibFiE4  

Shirika la umeme Tanzania laeleza nia yake ya kuwabana wanaoendesha shughuli za kuchomea vyuma kwenye makazi ya watu.https://youtu.be/DI3_7Kedo_w  

Chuo cha mafunzo ya kijeshi TMA chaingia makubaliano na chuo cha uhasibu Arusha kuanzisha shahada maalum ya sayansi ya kijeshi.https://youtu.be/FQ3g_DlfrnI  

Waziri mkuu asema serikali imejipanga kuwashughulikia wakurugenzi na wakuu wa idara watakao tumia vibaya fedha za umma.https://youtu.be/4MGxAOqdpNs  

Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mdogo katika majimbo ya Masasi na Ludewa lafikia tamati huku changamoto kadhaa zikiibuka katika baadhi ya vituo. https://youtu.be/pixekJRC95A   

Baadhi ya wachama wa Chadema jimbo la ubungo wamtaka Rais Magufuli kuwa makini na tume itayoundwa kumchunguza aliyekuwa mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni. https://youtu.be/FK5dOpNrWfA  

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko kuu Tabora mjini walalamikia kufanya kazi katika mazingira yasiyo ridhisha kiafya huku wakidai kero hiyo imedumu kwa miaka 10. https://youtu.be/_4j0l_QBYek  

Serikali imetakiwa kuvifunga viwanda vyote vinavyotengeneza mifuko ya plastic ili zoezi la kupiga marufuku matumizi ya mifuko hiyo lifanikiwe.https://youtu.be/5paHodiyXOA  

Serikali yasema haitasita kuwachukulia hatua kali wakurugenzi wa halmashauri watakaotumia vibaya fedha za miradi ya serikali;https://youtu.be/o3VQLL1_evc  

Serikali imewataka watanzania wanaotaka kuwekeza katika masuala ya gesi hapa nchini wajitokeze kuliko kuendelea kulalamika;https://youtu.be/IBs2F4XXbbY  

Wanachama wa CCM mkoani Dodoma wameiomba serikali kuharakisha kupeleka msaada wa chakula kwa wananchi waliokubwa na baa la njaa;https://youtu.be/fHZkihghAp0  

Watoto zaidi ya 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi leo wamefanyiwa upasuaji katika hosptali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/Q9PRYgK28K0  

Msaada  wa fedha  wa shilingi milioni moja alioutoa Rais John Magufuli  kutoka kwenye mshahara wake kwa mtoto Baraka mwenye Ulemavu anayeishi mkoani Mara umekabidhiwa hii leo; https://youtu.be/92AJg2AjsdM  

Klabu ya Azam imeibuka kidedea kwa kuitandika klabu ya Maji Maji ya mkoani Ruvuma jumla ya goli 2-1 katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu Tanzania bara; https://youtu.be/L3kXem6h-QM  

Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Burundi, Hamis Tambwe anayekipiga ndani ya klabu ya Yanga amesema mgogoro wa kisiasa uliopo nchini kwao hawezi kuuweka kichwani; https://youtu.be/hLncqWp7vEM

No comments: