Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigului Nchemba akiangalia Ng'ombe walio uwawa katika Mgogoro wa wakulima na Wafugaji katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero, katika tukio lililotokea Desemba 12 mwaka huu.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigului Nchemba akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Beth Mkwasa wakiwajulia hali watu waliojeruhiwa katika mgogoro wa wakulima na wafugaji uliotokea katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigului Nchemba akizungumza na
Mkuu wa wilaya Mvomero, Beth Mkwasa katika kijiji
cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu, walipotembelea katika kijiji hicho na kuona madhara makubwa yaliyojitokeza katika mgogoro wa wakulima na wafugaji. Nchemba alimwagiza Mkuu wa wilaya Mvomero, Beth Mkwasa kuunda kamati ya Ulinzi na Usalama katika wilaya ya Mvomero ili kamati ihusike maeneo yote ya Nchi yetu ili kuhakikisha wanaimarisha ulinzi maeneo yote yenye migogoro, pia wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigului Nchemba akizungumza wanachi wa kijiji cha Dihinda waliokusanyika katika eneo lililotokea mauaji ya wanyama na baadhi ya watu kujeruhiwa.
"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, kuwa hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote yule, njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa Serikali wa eneo husika hatua kwa hatua, Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi, t
unakwenda kuunda kamati za usuruhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria."
Alisema Nchemba.
No comments:
Post a Comment