Tuesday, December 15, 2015

Balozi Dkt. Mahiga akutana na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba waliwasili Wizarani kuanza kazi rasmi siku ya Jumamosi tarehe 12 Desemba 2015. 

Viongozi hao wapya wa Wizara walipokelewa na watumishi kwa shangwe walipowasili wizarani, muda mfupi baada ya kula kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Dar es Salaam.


Siku ya kwanza Wizarani, Waheshimiwa Mawaziri walipata fursa ya kukutana na uongozi wa Wizara ukiongozwa na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula na Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Joyce Mapunjo. Makatibu Wakuu hao pamoja na mambo mengine, walikabidhi kwa Waheshimiwa Mawaziri nyaraka muhimu za Wizara zitakazowaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao.


Aidha, walitumia fursa hiyo kueleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara na masuala ambayo yanahitaji miongozo yao ili yaweze kufanyiwa kazi na kukamilishwa.


Balozi Mahiga na Dkt. Kolimba walipata fursa pia ya kutembelea watumishi wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki siku ya tarehe 14 Desemba 2015 kwenye Jengo la Waterfront. Watumishi hao kama walivyofanya wenzao waliwapokea viongozi wapya kwa shangwe na baadaye kufanya kikao na Wakuu wa Idara na Vitengo.


Katika vikao vyote, Mhe. Waziri aliomba ushirikiano kutoka kwa Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wote kwa jumla ili kwa pamoja waweze kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye kaulimbiu ya “Hapa kazi tu”
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula aliyesimama akitoa neno kabla ya kumkaribisha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) kuongea na Wakuu wa Idara/Vitengo wa Wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na KimataifaMhe. Dkt. Suzan Kolimba
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi, Bw. Wilfred Masanja (wa kwanza kulia), na Kaimu Mkuu wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. John Ngowo wakisikiliza kwa makini neno la ukaribisho kutoka kwaBalozi Mulamula akimkaribisha Mhe. Waziri kuzungumza na Wakuu wa Idara/Vitengo.
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi walioudhuria kikao hicho, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Negel Msangi, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Balozi Anisa Mbega (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent Shiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki Bi. Grace Martine (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya, Bi. Tunsume Mwangolombe (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Eva Ng'itu nao wakiwa kwenye mkutano wa Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Dkt. Kolimba (hwapo pichani).
Sehemu nyingine ya Viongozi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Samuel Shelukindo, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bw. Marthias Abisai (wa kwanza kushoto), na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Nassoro Msumi (katikati).
Kikao kikiendele ========Kikao na Uongozi wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki========
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kutoka kushoto), na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzani Kolimba (wa kwanza kushoto) wakimsiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Joyce Mapunjo (wa pili kutoka kulia) katika kikao baina ya Mhe. Waziri na Wakuu wa Idara na Vitengo, wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mwingine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Amantius Msole.
Mhe. Joyce Mapunjo akiwatambulisha Wakurugenzi wake (hawapo pichani) kwa Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Waziri Kolimba
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulinzi na Siasa Bw. Amani Mwatonoka akijitambulisha kwa Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Waziri Dkt. Kolimba (hawapo pichani).
Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wakifuatilia kwa makini kikao kilichokuwa kinaendelea.
Makatibu wa Mawaziri nao wakifuatilia kwa makini mkutano huo, wa kwanza kushoto ni Bw. Thobias Makoba, na Adam Isara (wa kwanza kulia).
Kikao kikiendelea
Picha na Reginald Philip

No comments: