Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akihutubia Bunge la Jamhuri kama ishara ya kuzindua Bunge la 11.
Kabla ya Rais Dkt. Magufuli kuzindua Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju aliomba Bunge likubali kutenguliwa kwa kanuni za Bunge ili kuruhusu wageni kuingia ndani ya Bunge hilo.
Baada ya Mwanasheria Mkuu kutoa hoja Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akawahoji wabunge.
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiomba mwongozo wa Naibu Spika kwa kile alichodai kuwa kanuni zimekiukwa.Hata hivyo, kiongozi huyo wa Bunge alitoa mwongozo na baadaye alisitisha Bunge kuwaruhusu wageni kuingia kwenye ukumbi wa Bunge.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Jaji Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho wakiingia kwenye ukumbi wa Bunge huku wakiongozwa na mpambe wa Bunge.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (mwenye tai nyekundu katikati) akisindikizwa na wapambe wa Bunge kuingia kwenye ukumbi wa Bunge.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akimuongoza Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuingia kwenye ukumbi wa Bunge huku akisindikizwa na wapambe wa Bunge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Mgufuli akiingia Bungeni huku akiongozwa na Spika wa Bunge Job Ndugai na kusindikizwa na wapambe wa Bunge.
Baadhi ya wabunge wa upinzani wakiteta jambo wakati wageni wakiingia Bungeni.
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakifuatilia yanayojiri Bungeni.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson (kushoto), Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Jaji Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho wakiingia kwenye ukumbi wa Bunge huku wakiongozwa na mpambe wa Bunge.
Baada ya viongozi hao kuwasili kwenye ukumbi wa Bunge, wabunge wa Upinzani waliendelea kupiga meza na kuimba, hali iliyofanya ukumbi wa Bunge ukose utulivu.
Spika Job Ndugai akatoa amri ya kuwataka wabunge hao kuwa watulivu na walipokaidi amri hiyo akatoa amri ya kuwataka watoke nje ya ukumbu wa Bunge.
Wabunge wote wa upinzani wakatoka nje ya ukumbi wa Bunge isipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalende,Zitto Kabwe aliendelea kubaki ukumbini.
Hapa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akaanza kuhutubia Bunge.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Marais wastaafu, wakuu wa vikosi vya majeshi ya Ulinzi na Usalama, Maspika wastaafu, Watendaji Wakuu wa Serikali, Mawaziri Wakuu wastaafu na wageni wengine wakisikiliza hotuba ya Rais.
Baadhi ya wakuu wa mikoa, viongozi wa dini na wageni wengine waalikwa wakimsikiliza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Wabunge walionesha kuridhishwa na hotuba ya Mhe. Rais Makufuli, wakipiga meza kuunga mkono hotuba hiyo.
Baadhi ya Mabalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mhe. Rais Magufuli.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akitoa hotuba ya kuahirisha Bunge hadi mwezi Januari mwakani baada ya Mhe. Rais kulizindua Bunge hilo.
Baada ya kukamilika kwa kazi hizo, Mhe. Rais Magufuli akasindikizwa na wapambe wa Bunge kutoka nje ya Bunge huku akiambatana na Spika wa Bunge Job Ndugai.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli (wa pili kushoto) akiwa na Marais Wastaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia), Benjamin Wiliam Mkapa (kulia) na Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto).
Mhe. Rais Dkt. Magufuli (wa tatu kulia) akiwa na Spika wa Bunge Job Ndugai, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia kwake) na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) na Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Amani Abeid Karume (kulia).
Picha na Hussein Makame-MAELEZO
No comments:
Post a Comment