Saturday, November 21, 2015

KONGAMANO LA MABADILIKO YA TABIANCHI LAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO,JIJINI DAR

 Mc katika kongaman0 la Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu
 Eva Mageni  ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, akifungua kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alizungumzia kwa kifupi kuhusu mkutano wa COP21 ambao utafanyika Paris Ufaransa hivi karibuni.
 Edward Tunyone kutoka Forum CC akieleza maana zaidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alielekeza mazungumzo yake katika majanga asilia, mito kupotea kutokana na shughuli za wanadamu kama kulima jirani na maeneo hayo, mwisho alisisitiza swala la mabadiliko ya Tabianchi ni jukumu la kila mtu na taasisi zinazohusika na mamswala hayo tu.
 Bi Mwindiwe makame aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kutoka Zanzibar, akiendelea kueleza maana ya Mabadiliko ya Tabianchi alisisitiza kutunza mazingira.
 Denis Allan kutoka Norwegian Church Aid Actalliance akielezea umuhimu wa kutunza miti.
 Kikundi cha Ngonjela wakiendelea Kuburudisha
 Kushoto ni Mtaalam wa Mitandao ya kijamii toka Forum CC akitoa maelekezo ya shindano la Instagram
 Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza
 Aliyewahi kuwa Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 St.Matha akielezea jambo kuhusiana na mabadiliko ya Tabianchi
 Bw. Gambaedya P.M kutoka Tume ya Ardhi akitoa somo juu ya kilimo hifadhi
 Bi.Tatu Kayumbu kutoka Wizara ya Kilimo akieleza ushirikiano wa kilimo na utunzaji wa Mazingira
 Kundi la Youth can wakiendelea kutumbuiza
 Meneja wa Kampeni Haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akitoa mwongozo wa kikao
 Mkutano wa Forum CC ukiendelea
 Baadhi ya washiriki wakijadili Michoro ambayo walipewa kazi ya kuipitia na kuijadili.
 Baadhi ya washiriki wakielezea michoro waliyopewa kuielezea
Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akijumuika na wananchi wengine katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi
 Baadhi ya waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kwa nyakati tofauti wakionesha bidhaa zao
Kushoto ni mmoja wa washiriki waliohudhulia kongamano la mabadiliko ya Tabianchi akipokea zawadi ya tsh 100,000 aliyoshinda Steven Albert.
Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi

*******
ASASI za Kiraia nchini zikiwemo Oxfam Tanzania, Forum CC na Norwegian Church Aid Actalliance  zafanya kongamano  la Kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula nchini.

Akizungumza  Afisa Miradi Msaidizi wa Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema kuwakilisha sauti za wakulima  kwa serikali katika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Alisema  asilimia kubwa ya wakulima wengi hasa wanawake ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo wakati wanapolima.

Sawaya alisema  wananchi wanapaswa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo mbalimbali vya maji  ili kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

"Kwa kushirikiana  na shirika la Oxfam pamoja na Norwegian Church Aid  tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza bajeti,"alisema Sawaya
Aidha alisema asilimia kubwa ya wanawake wameonyesha juhudi mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha katika uzalishaji wa chakula.

"Tuwaunge mkono wazalishaji wa chakula wadogo,wafugaji pamoja na wavuvi  katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na kuwapa mikopo,"alisema

Aidha Kongamano  hili limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.

"Kongamano hili ni sehemu ya maandalizi ya  Mkuu wa  21 wa Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,"alisema Sewaya

No comments: