Saturday, November 21, 2015

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI


Wananchi zaidi  ya 500 wa kata ya Nyarugusu Mkoani Geita waandamana hadi zahanati ya kata hiyo wakishinikiza kuondolewa kwa wahudumu wa zahanati hiyo kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mama mjamzito.https://youtu.be/kF6wJDt_BIo
Hatua ya kwanza ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yaelezwa kukamilika kwa asilimia 65. https://youtu.be/Z-PW1LOT9bA

Zaidi ya shilingi bilioni 3 zimetumika katika ujenzi wa stendi mpya Kisasa ya Msamvu Mkoani Morogoro na kupelekea mradi huo kukamilika kwa asilimia 50. https://youtu.be/L05t_EvTLbU

Zaidi ya wajasiriamali 2,400 wa vikundi 18 wa vyama vya kuweka na kukopa SACCOS na vyama vya ushirika mkoani Simiyu wanufaika na mfuko wa taifa wa bima ya afya. https://youtu.be/BE0J-k1J44U

Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka maeneo ya msitu wa hifadhi wafanikiwa kukomesha uharibifu uliokuwa ukifanyika ndani ya hifadhi hiyo. https://youtu.be/cEv_X92zX3s
Imeelezwa kuwa Tanzania ni moja ya nchi amabazo watu wenye ulemavu wa ngozi(Abino) hufariki kutokana na matatizo ya saratani ya ngozi ikilinganishwa na nchi nyingine duniani. https://youtu.be/9evgLCkkCIQ

Operesheni ya ubomoaji wa nyumba na mabanda yaliyojengwa kinyume cha sheria yaendelea kwa siku ya tatu katika eneo la Mbezi beach wilayani Kinondoni. https://youtu.be/ynnbi9sm8ZY

Raisi Magufuli afungua rasmi bunge la 11 la jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akisisitiza serikali yake kudhibiti urasimu na kubana matumizi yatakayoendana na hali halisi ya kiuchumi. https://youtu.be/6aqzfTPXIhw
Baada ya tukio la hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa, baadhi ya wageni katika hafla hiyo watoa maoni yao juu ya uteuzi wake. https://youtu.be/Jtz_0Qrhrdc

Kufuatia hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, baadhi ya wananchi wa jimbo lake la Ruhangwa watoa maoni yao juu ya uteuzi wake. https://youtu.be/WPbz-oiOxD0

Mjadala mzito waendelea kutanda juu ya kitendawili cha aina ya baraza la mawaziri litakaloundwa na Raisi Magufuli huku wananchi na wabunge mkoani Dodoma wakitoa maoni yao juu ya baraza hilo.https://youtu.be/y3Q9iAPsXF4

Mawaziri wakuu wastaafu,Bw.John Malecela na Jaji Warioba watoa maoni na mtazamo wao juu ya uundwaji wa serikali mpya. https://youtu.be/7LW8IX2pGHY

TAMWA yataka mabadiliko ya demokrasia nchini kwa kutoka demokrasia ya chama hadi ya watu kufuatia malalamiko ya watu juu ya uteuzi wa wabunge viti maalum. https://youtu.be/kwyu4VSWO3E

Ukosefu wa elimu ya namna ya kuishi na watu wenye ulemavu wa ngozi(ALBINO) watajwa kuwa moja ya chanzo cha ongezeko la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi barani Afrika. https://youtu.be/Sl2YoeFPenA

Baraza la taifa la usimamizi na uhifadhi wa mazingira(NEMC) mkoani Mwanza lavifungia viwanda viwili mkoani humo na kuvitoza fani ya shilingi milioni 85, kwa makosa ya kukiuka sheria za uhifadhi wa mazingira.https://youtu.be/7z01YQrUVw8

Mtangazaji na mtayarishaji maarufu wa vipindi vya redio, Prince Baina Kamukuru afariki dunia baada ya kuaguka gafla wakati akifanya mazoezi jijini Dar es salaam. https://youtu.be/hIwsk6jYW88

Mtandao wa wanawake na katiba nchini walaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya wabunge cha kumzomea Mhe.Tulia Mwansasu; https://youtu.be/FF1SmuBxe9k

Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu,watakiwa kuacha ulaghai;https://youtu.be/7J8M_PjfsZM
Jeshi la polisi Mkoani Mwanza limepiga marufuku mikusanyiko ya watu pamoja na maandamano kwa kuhofia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu; https://youtu.be/X6BRnZR0Sac

Watu wawili wamethibitika kufariki kwa ugonjwa wa kipindupindu Mkoani Kagera na kuzua taharuki kwa wakazi wa mkoa huo; https://youtu.be/zPDz-Qb7DqI

Wakulima nchini washauriwa kutumia teknolojia ya mbegu chotara zinazo stahimili ukame ili kupata mavuno mengi katika eneo dogo la ardhi; https://youtu.be/i8mrtTE4kZU

Wadau wa michezo nchini watoa maoni yao kuhusu timu za taifa za Kilimanjaro Stars pamoja na Zanzibar Heroes zinazoshiriki michuano ya kombe la Challenge nchini Ethiopia; https://youtu.be/fbqbrJReg00

Klabu ya Real Madrid itawaalika maasimu wao klabu ya Barcelona katika mwendelezo wa ligi kuu ya nchini Uhispania hapo kesho; https://youtu.be/upouVemeGoA

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameahidi kudumisha ushirikiano na wabunge katika kutimiza wajibu wa serikali kwa wananchi; https://youtu.be/5cSrNb_MhRU

Wakazi wa mkoa wa Katavi wameeleza kuwa hotuba iliyotolewa na Raisi magufuli, imeonyesha matumaini makubwa katika kuboresha uchumi wa Tanzania; https://youtu.be/TJTOfwIdsMo
Wakazi wa mkoa wa Morogoro wampongeza Mh.Raisi Magufuli kwa hotuba yake safi aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa bunge la 11 mjini Dodoma. https://youtu.be/CrR4E2OruG0

Raisi John Magufuli aamuru kiasi cha pesa kilichotolewa kwa ajili ya hafla ya wabunge kitumike kununua vitanda hospitali ya taifa ya Muhimbili; https://youtu.be/wtmAlo3OtzQ
Raisi Magufuli aahidi kuboresha miundombinu ya kiuchumi ili kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020; https://youtu.be/F3wtBxMp9eA

Wadau wa biashara nchini wampongeza Waziri mkuu mteule Mhe.Kassim Majaliwa na kuahidi kushirikiana pamoja katika kutekeleza shughuli za serikali; https://youtu.be/8RMg6WnM02I

No comments: