Dk. Adeline l. Kimambo(kulia) kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akitoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku mbele ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliofika kujadili changamoto wanazokabiliwa nazo hasa wanapokuwa wanatoa huduma kwa jamii kuhusu matumizi ya Tumbaku na kuwaomba wadau hao kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo waliyojiwekea.Katikati ni Dk Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA).
(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii (TPHA),Dk. Mashombo Mkamba akizungumza jambo wakati wa majadiliano ni kwa namna gani wanaweza kupunguza matumizi ya Tumbaku katika jamii unayowazunguka na hata kuwaomba wadau mbalimbali kushirikiana ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya matumizi ya Tumbaku hasa kwa watoto wadogo ambao ni nguvu kazi ya baadae.
Dk.Tulitweni Mwinuka kutoka manispaa ya Temeke akieleza changamoto wanazozipata pale wanapokuwa wanatoa elimu ya matumizi ya Tumbaku na kusisitiza changamoto kubwa wanayoipata ni wanasiasa kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa kuhofia kupoteza wapiga kura wao wakati wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment