Tuesday, November 17, 2015

“Afya bora inaanza na kifungua kinywa bora” wito kutoka hospitali za Apollo kwenye siku ya kisukari duniani 2015

Dk. Bhuvaneshwari Shankar, Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo.

Na Mwandishi Wetu,

Novemba 14 kila mwaka tunaadhimisha siku ya kisukari duniani ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya kisukari, matatizo yanayoletwa na huu ugonjwa na taarifa muhimu kuhusu kisukari.

Siku hii inabeba ujumbe mahususi kwa watu wote ulimwenguni. Kauli mbiu katika siku hii tokea 2014 hadi 2016 ni maisha bora na kisukari(healthy living and diabetes) na mwaka huu kuna mtazamo zaidi katika kuzingatia mlo kamili na kuanza kila siku na kifungua kinywa bora.

Kutoka katika shirika la kisukari Africa, Tanzania ni kati ya nchi 32 katika shirikisho hilo kwa viwango vya nchi zenye viwango vya kisukari duniani. Kulikuwepo na zaidi ya kesi milioni 1.7 za kisukari hapa Tanzania kwa mwaka 2014. Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria zaidi ya watu milioni 180 ulimwenguni wana kisukari, na hiyo takwimu inatarajiwa kuongezeka ifikapo mwaka 2030 kama hamna hatua yoyote itakayochukuliwa.

Kifungua kinywa bora na sahihi kitasaidia sana kiwango cha sukari mwilini kutokuwa juu sana wala chini sana na kukuweka vizuri kutokea asubuhi.

Katika maadhimisho ya siku ya kisukari dunia, kliniki ya sukari kutoka hospitai za Apollo imeandaa siku 2 za kupima na kuhamasisha katika kambi iliyopo hospitali za Apollo kuwaasa watu kuhusu mifumo na staili za maisha yao ili kujikinga na kisukari. Kambi hiyo itakuwa na; vipimo vya sukari katika damu, mchanganuo wa mafuta mwilini, na namna ya kuepuka kisukari ambapo hospitali za Apollo zitatoa somo kuhusu milo kamili kutoka kwenye timu yao ya wataalam wa milo. 

Wataalam hao watafundisha namna ya kujikinga na kisukari kwa kuzingatia milo bora, namna ya kudhibiti kiwango cha sukari mwilini na namna ya kupambana na kisukari kwa ujumla.

Kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma hiyo ya kisukari kupitia elimu ya mlo, Dk. Bhuvaneshwari Shankar Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo, ana lengo la kuwaelimisha watanzania kuhusu mambo muhimu wanapaswa kuyajua kuhusu kisukari na mlo kamili katika siku hii ya kisukari duniani.

Kula kwa afya ni silaha bora kujikinga na kisukari. Mazoezi ya mara kwa mara na mlo kamili vinasaidia sana. Hamna chakula mahususi au mfumo mgumu wa lishe unaohitajika.
Dk Bhuvaneshwari Shankar anatutia moyo kula milo mitatu kama inavyostahili kitu ambacho watanzania wengi hatufanyi hivyo.

“muda mrefu bila chakula kunafanya sukari kushuka, na utajikuta unakula chakula kingi ambacho kitapelekea sukari katika damu kutokuwa sawa. Alisisitiza
Ratiba nzuri ya chakula cha mtu wa kisukari kinatakiwa kiwe na mafuta kidogo, mboga mboga, katika siku ni muhimu. chakula kingi kinanafanya sukari ya mwili kutokuwa sawa. Angalizo linahitajika katika uchaguzi sahihi wa vyakula.

Katika chaguo sahihi la vyakula “Dk Shankar wa hospitali ya Apollo anasisitiza umuhimu wa watanzania kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa kufuata mlo sahihi.

chagua vyakula vyenye nyuzinyuzi, na kabohaidreti ndogo ni muhimu. Epuka bidhaa nyingi zilizochujwa nyuzi zake, ila chagua unga. Unga ulio na virutubisho vyote ni wa muhimu. Dhibiti kiwango cha mafuta kuingia  mwilini, na epuka mafuta yaliyotengenezwa.

Ule milo 3 kwa siku na vitafunwa hapo katikakati. Chagua milo yenye nyuzinyuzi sana zaidi ya ile yenye kabohaidrates, mbogamboga zenye stachi Epuka chokleti, barafu tamu zenye mafuta na sukari nyingi. Chagua samaki wazuri na kuku wakuchemsha sio kukaangwa na mafuta. Chagua maziwa yenye mafuta kidogo.

Dumisha uzito unaopaswa kwa kufanya mazoezi kwa kutembea na kula katika muda muafaka, alisisitiza  Dk. Shankar.

Kisukari ni ugonjwa unaoathiri watu katika umri wowote ambapo mwili unashindwa kutengenzea sukari ya kutosha au kushindwa kutumia inslulini iliyotengezwa hivyo kupelekea kiwango cha sukari mwlini kutodhibitiwa. Mwili wa mwanadamu unapata sukari kutoka kwenye sehemu kuu mbili; kwanza kutoka kwenye vyakula tunavyokula, pili kutoka kwenye ini linalotengeneza pindi unapokuwa hujala chakula. Mwili unabadilisha hii sukari na wanga kwenda na kuwa nguvu kwa kutoa homoni zinazoitwa insulin zinazotengenezwa na kongosho.

No comments: