Meneja Biashara kutoka shirika la Mzinga Morogoro Pingu Kamenyi akiwaeleza wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya Shirika hilo katika kipindi cha Miaka kumi ya Serikali ya awamu ya nne ikiwemo uzalishaji wa zana bora za kilimo na ujenzi zinazolenga kuwainua wajasiriamali wadogo ili waweze kuinua uchumi wao na wa taifa kwa ujumla. Wa pili kushoto ni Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe na wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe akitoa wito kwa watanzania kutumia bidhaa zinazozalishwa na Shirika la Mzingira ambalo ni moja ya Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa leo jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni Meneja Biashara kutoka shirika la Mzinga Morogoro Pingu Kamenyi.
Miundo mbinu ya umwagiliaji katika shamba la mpunga.
Moja ya Bwawa lililojengwa kwa ustadi na shirika la Mzinga.
Mashine ya kutengeneza matofali inayotumia umeme.
Mashine ya Kuchanganya Chakula cha Mifugo
Mashine ya Kupukuchua Mahindi.
Mashine ya Kukoboa Nafaka
Mashine ya
Kuranda Mbao.
Frank Mvungi-MAELEZO
Serikali kupita Wizara
ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeendelea kuwainua wananchi kupitia
shirika la Mzinga kwa kuzalisha zana za kilimo, ufugaji na Ujenzi
zitakazosaidia kukuza na kuongeza kasi ya uzalishaji wenye tija katika sekta
hizo.
Hayo yamesemwa na
Meneja biashara wa Shirika hilo jana jijini Dar es salaam Bw. Pingu Kamenyi wakati
wa mkutano na wandishi wa habari uliolenga kueleza mafanikio ya shirika hilo
katika kipindi cha miaka kumi ya Serikali ya Awamu ya Nne.
Akifafanua Kamenyi
amesema Serikali imepata mafanikio
makubwa kupitia shirika hilo kwa kutekeleza miradi mbalimbali kama vile Ujenzi
wa daraja la Mabwepande wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, Ujenzi wa nyumba za
Halmashauri ya Masasi mkoani Mtwara, Ujenzi wa jengo la utawala la Hospitali ya
Wilaya ya Morogoro na Ujenzi wa uzio wa Halmashauri ya Manispaa hiyo.
“Shirika la Mzinga
lilianzishwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi ili waweze kujikomboa kiuchumi ndiyo
sababu iliyopelekea kuanzishwa kwa kampuni Tanzu ya Mzinga inayotekeleza miradi
kama vile ya ujenzi. “Alisisitiza Kamenyi.
Shirika limekuwa na
ushirikiano mzuri katika kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali
nchini.
Baadhi ya taasisi hizo zinajishughulisha
na utafiti na maendeleo ni hapa nchini ni pamoja COSTECH, CoET, CAMARTECTIRDO lengo
likiwa kupata teknolojia za kurahisisha utendaji kazi katika shughuli
mbalimbali zinazolenga kuwainua wananchi kiuchumi.
Katika jitihada za
kupanua huduma zake, Kamenyi amebainisha kuwa shirika hilo limefungua vituo vya kuuza milipuko, silaha na risasi za
kiraia, na pia wameweza kufungua vituo vinne zaidi vya mauzo katika miji ya Mererani , Arusha , Shinyanga na Mpanda.
Naye Msemaji wa Wizara
ya Ulinzi Luteni Kanali Juma Sipe alibainisha kuwa shirika hilo ni Kitovu cha
maendeleo kwa kuwa lengo lake ni kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuhakikisha
wanapata zana bora za uzalishaji kwa gharama nafuu.
Pia Luteni Kanali Sipe
aliwaasa watanzania kutumia zana zinazozalishwa na shirika hilo na zile zinazozalishwa na shirika la Nyumbu
kwa kuwa zina ubora na zinalenga katika kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja
na Taifa kwa Ujumla.
Shirika la Mzinga
lilianzishwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China mnamo
mwaka 1971 kama mradi chini ya Makao Makuu ya Jeshi (MMJ).
Kuanzia tarehe 13
Septemba mwaka1974, mradi ulibadilishwa kuwa Shirika la Umma (Public
Corporation) kwa Tamko la Serikali No.219.
No comments:
Post a Comment