Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodrigues (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy msaada wa Vifaa vya mawasiliano (Cameras, printers na Computers) kwa ajili ya kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje.
Balozi Celestine Mushy, akizungumza na Bw. Alvaro Rodrigues muda mfupi kabla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kufanyika. Balozi Mushy alishukuru msaada huo ambao alisema umekuja wakati mwafaka ambapo Serikali ipo katika mikakati ya kuboresha mawasiliano na wadau wake.
Mazungumzo yakiendelea....
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, akisaini nyaraka ya makabidhiano kama ishara ya kupokea msaada huo.Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodrigues naye akiweka sahihi kweye nyaraka ya makabidhiano kama ishara ya kukabidhi rasmi msaada huo wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kitengo cha mawasiliano ya serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje.
Balozi Celestine Mushy akiwa ameshikilia moja ya vifaa vya msaada huo huku baadhi ya Maofisa kutoka Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wakishuhudia.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga, akipokea msaada huo kutoka kwa Balozi Mushy.
Balozi Mushy akiwa ameshikilia Video Camera iliyotolewa msaada na UNDP.
PICHA NA: REUBEN MCHOME.
No comments:
Post a Comment