Thursday, October 15, 2015

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WATENDE HAKI :TAWLA

Ofisa Uchaguzi na Utawala Bora wa Halmashauri ya Kisarawe, Constantene Mnemere, akizungumza na washiriki wa mdahalo wa amani wakati wa uchaguzi kwa watendaji wa Serikali za Mitaa,Polisi na watumishi wa Halmashauri hiyo jana.
Ofisa Habari wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Goodness Mrema, akielezea muongozo wa mdahalo wa amani kwa wenyeviti, watendaji wa serikali za mita na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani jana, wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi.
Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Sara Kinyaga, akiwasilisha mada mbalimbali wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Baadhi ya washiriki wakimpongeza Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) (kushoto) baada ya kuanzisha mjadala wa amani wakati wa uchaguzi mkuu, wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana.

No comments: