Thursday, October 15, 2015

TANZANIA YAJIANDAA VEMA NA USIMAMIZI WA URANI





 Picha mbali mbali za wajumbe na viongozi na wataalamu (washauri) kutoka shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) pamoja na wafanyakazi wa Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania wakiwa katika semina ya juu ya usimamizi wa sheria na kanuni za usimamizi wa mionzi ya nyuklia Tanzania, iliyofanyika makao makuu ya Tume ya Mionzi Tanzania yaliyopo jijini Arusha. Picha na Yohana Challe.

NA; YOHANA CHALLE ARUSHA.
TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), imesema kuwa imejiandaa vilivyo katika usimamizi wa uchimbaji wa madini ya urani ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia John Mngodo alisema kuwa moja ya majukumu ambayo serikali inafanya ni kujiandaa juu ya kusimamia uchimbajia wa madini hayo.

“Mkazo uliowekwa hapa ni kwamba ni lazima usalama wa mionzi upewe mkazo hivyo TAEC itahakikisha usalama unakuwepo na katika kila hatua ambayo watakuwa wanajiandaa au wanachimba na kusafirisha madini ya urani lazima ukaguzi ufanyike na kutoa kibali ili kuhakikisha usalama unakuwepo” alisema Mngodo.

Mngodo alizungumza hayo wakati wa kuhitimisha zoezi la kupitia taratibu za uendeshaji, ukaguzi na usimamzi wa nyuklia na mionzi hapa nchini, zoezi hili lilifanyika kwa siku kumi tangu Oktoba 4 hadi oktoba 14 mwaka huu katika makao makuu ya Tume hiyo mkoani hapa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka zaidi ya nchi 10 duniani.

“Wataalamu hawa walikuwa wakipitia taratibu na namna ya jinsi ambavyo tunavyosimamia shughuli za mionzi na nyuklia hapa nchini” alisema Mngodo.

Wataalamu hawa wametokea katika nchi za Jordani, Irend, Ubelgiji, Sudani, Kenya,Ukreini, Argentina, Australia, Pakistani, Nigeria, Zimbabwe, Uingereza na Zambia

Wataalamu hawa walikuja kwa mwaliko wa serikali ili kuweza kuisaidia Tume hii ili kuweza kuboresha zaidi shughuli zinazoendelea hasa elimu kwa wafanyakazi, pamoja na kupitia sheria na kanuni za usimamizi wa masuala ya Nyuklia na mionzi hapa nchini.

Aliongeza kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni jinsi ya kuwapata wataalamu wa kusimamia shughuli hizo (rasilimali watu) pamoja na fedha, japo akiipongeza serikali kwa kuendelea kujitahidi kutoa mafungu ili kuendelea kuboresha shughuli za Tume.

Kwa upande wake Leonard Kifanga ambaye ni Mwanasayansi mwandamizi wa nyuklia, alisema kuwa lazima Tanzania iwe na mipango mikakati ya kuboresha na kushughulikia ajali za kinyuklia zinazoweza kujitokeza, kwani itasaidia kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kuepukika kwa urahisi na kwa haraka.

“Nashauri lazima Tume na Taasisi za kusimamia majanga ziwe huru ili zifanye kazi kwa uhuru zaidi na kwa haraka ili kila mtu aweze kuwajibika katika nafasi yake na hii itasaidia kujua tatizo lilipoanzia” alisema Bwana Kifanga.

Kifanga ni mmoja wa waatalamu kutoka nchini waliokwenda japani kwenye uchunguzi wa mlipuko wa kinu cha nyuklia cha Fukushima kilichotokea baada ya kutokea tetemeko la ardhi lililoharibu mfumo wa kinu cha nyuklia na hatimaye kinu kupasuka na kutokea mlipuko.

No comments: