Sunday, October 18, 2015

TAMASHA LA KANDANDA DAY LAFANYIKA LEO JJINI DAR ES SALAAM

 Mgeni rasmi  Angetile Osiah akizugumza katika  Tamasha la Kandanda Day 2015, hufanyika kila mwaka mwezi oktoba kwa kuzikutanisha Team Ismail  (Blue Jersey)na Dizo Moja (White Jersey) lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara, leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Patrick Dumulinyi  akisisitiza jambo katika tamasha hilo.
 Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres, Nassor Binslum, akionesha makeke yake uwanjani wakati wa Tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu  Ismail wakionyesha furaha ya ushindi Tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi  Angetile Osiah akiwa na wanakamati wa timu katika picha ya pamoja katika  Tamasha la Kandanda Day 2015, Lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara, leo jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi  Angetile Osiah akimkabidh kombe captain Ismail Mohamed  katika  Tamasha la Kandanda Day 2015, Lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres, Nassor Binslum, akipima afya wakati wa Tamasha hilo.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya Jamii)


TAMASHA la Kandanda Day 2015, Lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara,ambalo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba kwa kutanisha Team Ismail  (Blue Jersey) na Dizo Moja (White Jersey).

Mwaka jana Team Ismail ilipoteza kwa bao 4-1, na mwaka huu Team Ismail imeibuka kwa ushindi wa bao 2-0.

Mbali na mchezo huo Wakandanda walipata nafasi ya kupima Afya zao kupitia Chama cha Madaktari  Wa Michezo Tanzania, (TASMA), pia kulikuwa na mauzo ya Tshirts ambazo zinachangia mfuko wa MpiraMmoja, KitabuKimoja kwa shule na vituo vya watoto. Hivyo katika kila mwanakandanda aliekuwa amevaa T-Shirt ya Kandanda Day alikuwa mechangia mfuko huu.

Kwa wale ambao walikuja na magari yao, waliwekewa Tiketi  yenye Muhuri na Namba ya Gari, watatkiwa kwenda na karatasi hizo katika Duka la Mac Auto Accessories  watapata discount ya asilimia 10% kwa huduma zao

No comments: