Bi. Bahati Muriga alifika Ubalozi wa Tanzania, Washington DC kuhudhuria tafrija iliyoandaliwa na Oxfam America. Bi. Muriga aliongelea maisha yake katika Mkoa wa Mwanza alipokuwa anafanya kazi kama Mkuu wa shule ya msingi, pamoja na hayo pia aliweza kuingia katika shughuli za kilimo akitafuta kipato ya kusomesha watoto wake wawili ili kuwapatia maisha bora.
Ubalozi wa Tanzania Washington DC ulipata ugeni wa wasau kutoka mashirika mbalimbali waliokuja kuungana na Oxfam America inayoandaa Siku ya Chakula Duniani “World Food Day 2015” tarehe 16 Octoba. Bi. Muriga atasafiri kwenda katika mji wa Des Moines, Iowa kushiriki katika ziara na Oxfam inayoandaa matamasha mbalimbali kama ya “World Food Prize”.
Bi Bahati Muriga akielezea ni jinsi gani alivyo na furaha kufika ubalozini na kuweza kukutana na watu mbalimbali kutoka mashirika tofauti hususan OXFAM.
Bi Bahati Muruga akiwa pamoja na mwenyeji wake wa jioni hiyo Afisa ubalozi Suleiman Saleh.
Wageni mbalimbali waliweza kuhudhuria na kuchanganyika pamoja na wenyeji wao ambao ni wafanyakazi wa ubalozi Pichani ni Mayor Mlima pamoja na Alice .
No comments:
Post a Comment