Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani
Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika
mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao
waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa
muda katika kambi ya Nyarugusu.
Wakimbizi kutoka nchini Burundi wakipanga mizigo yao katika
kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wamehifadhiwa kwa muda
kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati
unaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la
Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya
kimataifa ili kuwapatia makazi salama.
Mtoto Jamine Nibetanga(14), kutoka nchini Burundi akiandaa
chakula katika kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka
nchini Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za
Nduta, Karago na Mtendeli.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Kukimana Dafroza (katikati),
akifuma kikapu kama alivyokutwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B
iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka Burundi
wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa katika kambi nyingine. Wengine ni
Mkabanura Eviline (kushoto) na Niragira Dafroza (kulia).
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wakichota maji
jana katika moja ya vituo vya maji vilivyowekwa katika kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa
muda. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
ina mpango wa kuwahamishiwa katika kambi za Karago, Mtendeli na Nduta ili
kupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenye
mtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa
huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma. Shirika la Red Cross ni mojawapo ya wadau wanaoshirikiana
na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.
Mkimbizi Joseph Mtagura aliyeko katika Kambi ya Wakimbizi ya
Nyarugusu akiandaa mihogo ya kuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi
ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Ntirampeba Acquelina
akianika mihogo ambayo huwauzia wenzake
katika kambi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Ugali
wa mihogo ni mojawapo ya vyakula muhimu
vinavyotumika katika kambi ya Nyarugusu.
Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaohifadhiwa
katika kambi ya Nyarugusu wakicheza mpira kama walivyokutwa jana na mpiga picha
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wakimbizi hao wamekua wakiingia nchini kutokana na machafuko ya kisiasa
yaliyotokea nchini Burundi hivi karibuni.
Wakimbizi kutoka Burundi walioko katika Kambi ya Nyarugusu
wakiandaa mboga ya kisamvu kama walivyokutwa na mpiga picha wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi aliyeko katika ziara
katika kambi hiyo.
Mkimbizi Haverimana Ejide (kushoto) na mkewe Kugimana Evona
pamoja na watoto wao wakipata chakula cha mchana katika kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda
kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ili kupunguza msongamano uliopo katika
kambi ya Nyarugusu.
(PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI)
1 comment:
NA SISI WATANZANIA TUKIVURUGA AMANI TUTAKUA KAMA HIVI. TUSHUKURU TUPO MAJUMBANI KWETU TUNAKULA NA KULALA
Post a Comment