Na Beatrice Lyimo –
Maelezo
12/09/2015
SERIKALI imewataka Serikali
imetoa changamoto kwa watendaji wote afya wa
halmashauri ,mikoa wilaya kuhakikisha wanabuni mbinu mpya na kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza
kuendelea kuboresha huduma za sekta ya afya nchini.
Aidha Serikali pia imewataka watendaji wa Idara ya Ustawi wa
Jamii, kujumuisha suala la kutatua tatizo la watoto yatima kwa kuweka katika mipango
ya sekta hiyo.
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati
akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa sekta
ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8
hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.
“Kila
mmoja anapaswa kusimamia vyanzo vya
mapato, misaada na bajeti ya Serikali haikidhi mahitaji kwa asilimia 100. Tunapaswa
kusimamia kwa ukamini na ukamilifu suala la mapato katika vituo vya afya.
Tusipotekeleza wajibu wetu ipasavyo tutawajibika kwa hili tutawajibika kwa
Watanzania na hata kwa Mwenyezi Mungu,” alisema Dkt. Mmbando.
Aliongeza kwamba hili kuweza kufanikiwa vema katika
masuala hayo wanapaswa kuwa makini katika kutoa maelekezo kwa kuzingatia sera,
taratibu, miongozo na mikakati rasmi ya
Sera ya Afya ya mwaka 2007.
Aliwataka watendaji hao, kushirikiana pamoja
katika kutatua changamoto mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kuwasiliana na
uongozi wa wizara.Pia kutumia uzoefu walioupta katika mkutano huo.
Kwa upande
wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI), Dkt. Deo Mutasiwa alisema watendaji hao kuongeza kasi ya
utendaji kazi ili kuweza kukabiliana na matatizo ya sekta ya afya nchinina
kufanikisha malengo ya milinea(MDG’s), mkakati wa awamu ya nne wa afya,
kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na mamawajawazito, kutoa elimu juu
ya masuala ya lishe kwa jamii.
No comments:
Post a Comment