Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Deo Mutasiwa asisitiza jambo jana
jioni wakati wa ufungaji wa mkutano mkuu
wa mwaka wa sekta ya afya ambao
uliambatana na maadhimisho ya miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba
8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando na wakipongezana mara baada ya kumaliza jana jioni mkutano mkuu wa mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na
maadhimisho ya miaka 40 ya Mpango
wa Taifa wa Chanjo uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba
8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.
Picha namba
3367 ni Baadhi ya wanganga wakuu wa mikoa na wilaya wakiwa katika huo.
Na Magreth Kinabo
SERIKALI imewataka watendaji
wote afya wa halmashauri ,mikoa wilaya kusimamia suala la usafi wa mazingira ilikuizesha
jamii kuepukana na matatizo ya milipuko ya magonjwa likiwemo suala la ugonjwa
wa kipindupindu.
Aidha Serikali pia
imewataka watendaji hao, kuanzisha siku maalum ya usafi katika maeneo
wanayotoka.
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati akifunga mkutano mkuu
wa mwaka wa sekta ya afya ambao
uliambatana na maadhimisho ya
miaka 40 ya Mpango wa Taifa wa
Chanjo uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8
hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.
“Ni lazima tuwe na utaratibu huu mpya kwa kushirikiana na
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)
vyombo vya habari ili kuweza kutatua tatizo hilo,” alisema Dkt. Mmbando.
Aliongeza kwamba
watendaji hao watakiwa kutoendelea kuruhusu vyakula kusafirishwa katika maeneo
ya wazi, madimbwi ya maji machafu, usimamizi wa huduma za afya ufanyike
ipasavyo.
“ Tusimamie mpango wa utekelezaji wa elimu ya afya
mashuleni, likiwemo suala la vyoo ambalo limepewa walimu maalum wa kusimamia
,hivyo zamani tulikuwa tunakaguliwa kuhusiana na usafi wa mwili mashule mafano
kuoga nna kuchana nyewele pia kuweka
yanayotunguzuka kuwa safi mazingira. Turudi katika misingi hiyo
tuaondokana na matatizo ya afya,” alisisitiza.
Dkt. Mmbando alisema
kanuni na miongozi ipi ya kutosha hivyo, watendaji hao wanapaswa kuongeza kasi
ya utendaji kazi na kushirikiana kwa pamoja katika kukabiliana na magonjwa
yasiyoambukiza na kuambukiza ili kuweza kuiwezesha sekta ya afya kupata
mafanikio makubwea zaidi katika kufikia malengo ya milinea(MDG’s ).
Aliongeza kwamba Mlipuko wa magonjwa ya
kipindupindu umetokea katika mikoa ya Dares Salaam, Morogoro na Pwani na unatokana na tatizo la kutozingatia ,
misingi ya usafi wa mazingira husasan kwenye vinywaji, vyakula na mazingira
yasiyosafi.
No comments:
Post a Comment