Mkurugenzi
wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya
nchi, Abdulmaliki Mollel akitoa maelezo katika semina ya kuwajengea
uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China leo
katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
wakilipia tisheti kwa ajili ya sare ya kutambuana wakati wa safari
ya kwenda katika vyuo vya China katika semina ya kuwajengea uwezo
wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China leo katika
ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa
jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakipata maelekekezo mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi wa
Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi,
Abdulmaliki Mollel katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na
wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China.
Mkurugenzi
wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya
nchi, Abdulmaliki Mollel akibadilisha nawazo na wazazi walifika na
watoto wao wanaotarajia kwenda kusoma vyuo vya China.
Wanafunzi
wakiingia katika ofisi ya Global Education Link kupata maelezo
mafunzo ya wanafaunzi wanaokwenda kusoma vyuo vya China.
Wanafunzi wakiabadilishana mawazo mara baada ya kumaliza mafunzo yao leo, yaliyoendeshwa na GEL.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Education Link,Abdulmalik Mollel akizungumza na
wafanyakazi wake mara baada ya kumaliza mafunzo ya wanafunzi
wanaokwenda kusoma nchini China.
(Picha na Emanuel Massaka).
Na
Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Global Education Link (GEL) leo imeendesha mafunzo kwa wanafunzi
wanaokwenda vyuo vya China kwa ajili ya kuanza safari na mazingira
ambayo watayakuta katika vyuo hivyo.
Akizungumza
na katika mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wanafunzi 70 jinsi ya
kuanza safari ya masomo katika vyuo vya China wanaotarajia kuondoka
Septemba 22 mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Abdulmaaliki Mollel
amesema kuwa mafunzo hayo ni kuwaandaa wanafunzi jinsi ya kuanza safari
yao kuanzia uwanja wa ndege hadi katika vyuo wanavyokwenda.
Mollel
aliwataka wazazi kuwa waangalifu na matumizi wanayopewa wakiwa vyuoni
inapofikia inazidi inashawishi wanafunzi kufanya vitu visivyo na
kuweza kufanya asiweze kupata elimu ambayo mzazi alikuwa anatarajia
aipate huku nje.
Katika
Mafunzo hayo wanafunzi wamepewa nyaraka mbalimbali ambazo ni juu ya
vyuo hivyo ambazo ni Chuo anachokwenda kuidhinishwa na Tume ya Vyuo
Vikuu Nchini (TCU), Taarifa za nyaraka zenye alama za vidole kutoka
katika jeshi la polisi kuonyesha wanafunzi hao hawana makosa ya
kijinai.
Amesema
kuwa Global Education Link imekuwa ikifanya kwa niaba ya vyuo vya nje
ambavyo vina ubora wa kutoa elimu iliyobora ambayo itakuwa na tija kwa
taifa pamoja na yeye mwenyewe.
Hata
hivyo aliwataka wazazi kuwaandaa mapema watoto wao wanaokwenda kusoma
ili kuweza kuondokana na usumbufu ambao unaweza kufanya asiweze kwenda
huku akiwa ameshalipa ada pamoja na tiketi ya safari.
Aidha Mkuirugenzi Mtendaji amesema kuwa utaratibu wote wa kuondoka na
kufika katika vyuo hivyo anafanya ikiwa ni sehemu ya kuondokana na
usumbufu kutokana na wanafunzi hao baadhi ni wageni katika kusafiri na
ndege.
Mollel
amesema wanaokwenda kusoma nchini China wengi wao ni masomo ya uhandisi
wa Mafuta,Ndege,Ujenzi pamoja na udakitari kwa elimu juu waliomaliza
kidato cha sita.
Amesema
nafasi katika masomo ya elimu juu bado zipo wanachotakiwa ni nkufanya
mchakato wa mawasiliano wa kuweza kudailiwa hili ni moja ya makundi
ambapo mengine yalishaondoka.
Mollel
amesema kuwa nafasi zipo katika vyuo vya nje kutokana kuendelea
kufunguliwa kwa mawasiliano zaidi www.gel.co.tz na mawasilino ya simu
ni+ 255 656 200 200.
Aidha amewataka wazazi na wanafunzi kuacha kutumia baadhi ya watu walio
katika nchi mbalimbali zenye vyuo kudai wao ndio wanajua ni uongo
kwani Global Education Link ndio inaingia mikataba na vyuo vya nje na
wengine hawajaingia mikataba.
Kwa
upande Mzazi Dk. Nicholas Eseko amsema mafunzo ni mazuri kwa kuwajengea
uwezo wanafunzi wakti kuanza safari pamoja na mazingira watayoyakuta
katika vyuo hivyo.
Mwanafunzi
Ismail Michael amesema kuwa mafunzo ni mazuri yanatoa mwanga wa kuanza
safari ya kwenda katika vyuo hivyo vyenye ubora.
“Sisi wanafunzi tunafarijika kwa kupata mwanga jinsi ya kuanza safari
yetu na kujua vitu vibaya katika viwanja vya ndege ambavyo vinaweza
ukafanya uwe uingie katika mikono ya dola”amesema Michael.
No comments:
Post a Comment