Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili
katika uwanja wa CCM mjini Bariadi kwa ajili ya kuwahutubia kwenye
mkutano wa kampeni mkoani Simiyu.
Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi
Wananchi
wa Nanga wilaya ya Itilima wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa
CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia
Umati
wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika
kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo
Wananchi
wakimsiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufui alipokuwa
akiwahutubia mjini Meatu jioni ya leo.Dkt Magufuli leo ametembelea
wilaya ya Busega,Bariadi,Itilima pamoja na wilaya ya Meatu mkoa wa
Simiyu
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,
Dk.Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanhunzi jioni ya leo mjini
Meatu mkoani Simiyu,Dkt Magufuli alisema kuwa atakapokuwa Rais atakuwa
karibu na wananchi wanyonge na kuwa yeye anatoka katika familia ya watu
maskini na anajua nini maana ya umaskini,Alisema anatoka kwenye familia
ya wakulima na wafugaji hivyo anajua nini ambacho anatakiwa kufanya
kuboresha maisha ya makundi hayo mawili na kwenye hilo atahakikisha
anaweka mazingiza mazuri ya matumizi bora ya ardhi.
Alisema Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.
"Nitakuwa upande wenu wananchi wanyonge.Serikali yangu ni marufuku watu wa bodaboda kushikwa na polisi.Serikali yangu haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo.Hivyo sitakuwa tayari kuona mama ntile wanatozwa kodi.Najua nitaimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yangu lakini nitawabana wafayabiashara wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi,"alisema Dk.Magufuli.
Aliwataka wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.
Dk.Magafuli aliweka wazi anapenda mabadiliko yenye tija na kwamba Serikali yake itasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma ili wafanye kazi ya kuwatumikia waanchi usiku na mchana na ndio maana atawalipa vizuri na kuongeza hapendi watu wavivu kwenye kazi.

Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa
wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu
jioni ya leo.
Wananchi wa Mwanhunzi mjini Meatu wakifautilia mkutano huo wa hadhara wa kampeni.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge na
Madiwani kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mwanhunzi,mjini Meatu
jioni ya leo mkoani Simiyu.
Wakazi
wa Lamadi ndani ndani ya wilaya ya Busega,Mkoani Simiyu wakishangilia
jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini humo leo.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Busega,Raphael Chegeni akiwahutubia wananchi wa
Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika
uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
Mwenyekiti
wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha mgombea Urais
wa CCM Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa Busega,mapema leo mchana
kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa
Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli
akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi
wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika
uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi
wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika
uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.Dkt Magufuli
aliwaomba wananchi hao kuitunza amani waliyonayo na kuwa kuwapuuza wale
wote wenye maneno ya kuleta ufarakanishi katika nchi yetu
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha
Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa kijiji
cha Mkula,alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi hao akielekea Wilayani
Busega kwenye mkutano wa hadhara.
Maandalizi ya kumpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ndani ya uwanja wa CCM mjini Bariadi yalikuwa kama hivyo pichani.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa
Mwanhunzi,alipomaliza kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
uliofanyika jioni ya leo mjini Mwanhunzi,Wilayani Meatu mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment