Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus
Mgaya akizungumza na waandishi habari leo kuhusu kongamano la saba la
elimu ya juu 2015 linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba
1-2, 2015. Pembeni ni Thea Mtau (kulia) na Cosmas Mwasoibya ambao ni
wajumbe wa Kamati ya Maandalizi.
Waandsihi wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini
(TCU), Profesa Yunus Mgaya katika mkutano na waandsihi wa habari
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii/Picha na Cathbert Kajuna.
WIZARA
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu
nchini ,Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya
Wakuu wa vuo Vikuu nchini (CVCPT) imeandaa kongamano la saba la elimu.
Akizungumza
na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Tume
ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya amesema wazo la kuandaa
makongamano ya elimu ya juu nchini ni kubadilishana uzoefu na maarifa
miongoni mwa wadau elimu katika mstakabali wa taifa.
Amesema
katika makongamano watajadili changamoto zinazokabili sekta ya elimu ya
juu kutokana na kupanuka kwa sekta hiyo kwa kuwa uazishwaji wa vyuo
vikuu binafsi na ongezeko la udahili vyuoni na mabadiliko mengine.
Profesa
Mgaya amesema kongamano wanalotajia kulifanya ni la saba ambalo
linatarajia kufanyika Oktoba 1 hadi 2 mwaka huu mkoani Arusha.
Amesema
katika kongamano hilo lina malengo ya kuangalia jukumu la Taasisi za
Elimu juu nchini kusaidia maendeleo uwezo kwa kuzingatia elimu
inayotolewa, Kubainisha fursa muhimu amabazo taasisi ya elimu zinaweza
kutumia pamoja na mkakati wa itakayowezesha ushirikiano madhubuti
baina ya sekta binafsi ya elimu ya juu,Viwanda na wadau wengine wa
kuleta mabadilko katika sekta ya elimu nchini.
No comments:
Post a Comment