Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa (wa tano kulia),
akifurahi baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya
Biashara ya Bidhaa za China 2015, uliofanyika Ukumbi wa Karimjee Dar es
Salaam leo asubuhi. Wengine na maofisa biashara wa China na wadau wa
masuala ya biashara.
Hapa Katibu Uledi Mussa akitia saini wakati wa ufunguzi wa maonyesha hayo.
Hapa akioneshwa bidhaa mbalimbali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa, akizungumza na wanahabari.
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA
la Viwango Tanzania(TBS) limesema bidhaa zinazotoka china zina ubora
huku likitoa mwito kwa wafanyabishara kutumia fursa ya kujifunza kupitia
maonesho ya bidhaa za china.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo,
Joseph Masikitiko,Mkurugenzi wa biashara Agnes Mneney alisema haiwekani
kujua kma bidhaa zina ubora au la kwa kuangalia kwa macho.
Alisema
TBS ndio waliopewa dhamana na Serikali ya kukangua ubora wa bidhaa zote
za ndani na za nje kisha kubainisha kwa wananchi kama bidhaa zina ubora
au ni hafifu kwa maslahi ya taifa.
''TBS
ndio imepewa dhamana ya kudhibiti bidhaa zenye ubora kwa maslahi ya
taifa kwahiyo watanzania wasipende kutoa hukumu kwa njia ya kukaangali
kwa macho,''alisema.
Agnes
alisema mtanzania anachotakiwa kufanya ni kuhahakikisha ananunua bidhaa
ambazo zina nembo ya TBS kwasababu bidhaa zote sokoni zinatakiwa kuwa
na viwango vya shirika hilo.
''Bidhaa
za nchini China lazima ziwe na vuwango vya ubora vinavyotolewa TBS ili
kuzingatia kiwango cha ubora katika soko la Tanzania,''alisema.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa masuala ya biashara na uchuminchini China,Lin
Zhiyong alisema maoyesho ni ya siku tatu ambapo zaidi ya wafanyabishara
kutoka nchina 230 wameshawasili nchini.
Akizungumzia
ubora wa bidha zao,Zhiyong alisema kupitia udhibiti waTBS
wafanyabishara wa china wameanza kuondoa bidhaa ambazo ni hafifu sokoni.
''Bidhaa
hafifu zimeanza kuondolewa sokoni kwa takribani miezi mitatu iliyopita
ili kuimarisha ushirikiano wetu na TBS na mkakati wa wafanyabishara wa
China ni kuhakikisha tunaondoa bidhaa zote hahifu ili kulinda
bora,''alisema.
Kwa
upende wake Katibu Mkuu wa viwanda na bishara,Uledi Mussa alisema
Tanzania imekuwa na urafiki mkubwa wa masuala ya kiuchumi na China.
Alisema
kupitia urafiki huo ni imani yake China itaisaidia Tanzania kujenga
viwanda na kuisaidia Tanzania kuzalisha vitu vyenye ubora na kuviuza.
Mussa
alisema Tanzania inaanda mpango wa kuanzisha viwandana kwamba dhamira
ya wizara husika ni kuwawesha wafanyabishara wazawa kumiliki viwanda kwa
maaendeleo ya nchi.
''Tumekuwa
na mambo mengi lakini dhamira ya Serikali kwa miaka mitano inayokuja ni
kujenga viwanda na kuwezesha wafanyabishara wazawa
kuvimiliki,''alisema.
Maonesho
hayo ni ya nne tangu kuanza kuonyeshwa nchini ambayo yanaendelea kwa
siku tatu katika viwanja vya Daimond Jubilee jijini Dar es Salaam.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
No comments:
Post a Comment