Mkuu
wa Maabara
ya Mikrobilojia wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA)Dk. Adelard
Mtenga akitoa maelekezo juu
ya kifaa maalum cha uchunguzi wa Vifaa
tiba ikiwemo nyuzi za ushonaji pamoja na dawa za sindano ambapo ni
kifaa cha kwanza Katika Nchi za Kusini ,Mashariki na Kati Barani
Afrika. leo Jiji Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti
Sillo akikata utepe kufungua mtambo huo leo Jiji Dar es Salaam. Katiti
ni mwakilishi mkazi wa Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii Dk. Mohammed Ally
Mohammed kuli ni Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly
Hamblin.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti
akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly
Hamblin akifafanua jambokwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti
Sillo na Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly
Hamblin wakisani makabidhiano ya nyaraka
za mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Hiiti
Sillo na Mwakilishi wa Shirika la Msaada kutoka Marekani,Ms. Kelly
Hamblin wakisani makabidhiano ya nyaraka
za mradi huo.
Wanahabari wakichukua matukio kwenye hafla hiyo.
Viongozi hao wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya hafla hiyo.Picha na Emmanuel Massaka.
MAMLAKA ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) imezindua
jengo la maabara ambalo litatumika kufanya uchunguzi wa madawa vyakula na
vipodozi ili kubaini baadhi ya vijidudu hatarishi kwa afya ya binadamu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakati akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi na makabidhiano ya Maabara hiyo.
Alisema kuwa Dawa zinazofanyiwa uchunguzi ni zile
zinazoingia moja kwa moja kwenye mwili wa binadamu,ili kuhakiki kuwa ziko
salama na hazina chembechembe yoyote ya wadudu wenye kudhuru
afya za binadamu.
“Kifaa hiki kitasaidia kufanya uchunguzi kwa kiwango
cha kimataifa na pia hakitaruhusu chembechembe yoyote kupita kwenye dawa na
kuathiri afya ya binadamu”alisema.
Naye Mkurugenzi wa uhakiki wa Ubora wa huduma ya
afya kutoka Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii Daktari Mohamed Mohamed amesema
kuwa maabara hiyo inahitaji uangalizi wa kutosha ili kutunza vifaa katika
maabara pamoja na kutoa elimu kwa wataalamu wa maabara hiyo.
Ukarabati wa jengo hilo umegharimu jumla ya fedha za
kitanzania kiasi cha shilingi milioni 489,ambapo serikali ya Tanzania
imechangia kiasi cha shilingi milioni 91 huku shirika la misaada la
marekani(USAID) limegharamia shilingi milioni 398.
No comments:
Post a Comment