Waziri wa Afya Dokta Seif Rashid
Na: Neema Mwangomo, MHN
04 Sept 2015
Rais JAKAYA KIKWETE leo
amezindua Taasisi ya Moyo ambayo itajulikana kwa jina la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ( The Jakaya
Kikwete Cardiac Institute ) ambayo
itatoa mafunzo ya Ubingwa wa juu katika fani ya Upasuaji wa Moyo , Usingizi na
Tiba ya Moyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili( MUHAS).
Akizindua
Taasisi hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa
niaba ya Rais JAYAKA KIKWETE , Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta SEIF RASHID
amesema taasisi hiyo imeleta ahueni kwa wagonjwa wa moyo nchini ambapo kati ya Januari hadi Agosti
mwaka huu imehudumia wagonjwa wa nje 14, 257 ,wagonjwa waliolazwa ni 912 na
imefanya upasuaji kwa wagonjwa 148.
Kati ya wagonjwa waliofanyiwa
upasuaji ,wagonjwa watano tu ndio waliofariki Dunia ambao ni Asilimia 3. 4 ,
kiwango ambacho ni kidogo kuliko wastani uliokisiwa na wataalam wa asilimia 13.
Akifafanua amesema huduma
zilizotolewa na taasisi hiyo zimeokoa
kiasi cha Shilingi 1, 915,440,000 iwapo wagonjwa
hao wangepelekwa kutibiwa nje ya nchi.
Akielezea kuhusu hali ya magonjwa
yasiyo na maambukizi amesema magonjwa hayo hujumuisha magonjwa ya Moyo ,
Kisukari na Saratani na kwamba takwimu za Shirika la Afya Duniani ( WHO)
zinaonesha kuwa takribani watu Milioni 17 hupoteza maisha kila mwaka Duniani
ambayo ni sawa na asilimia 60 ya vifo vyote vinavyotokea.
Hata hivyo amesema sababu kuu ya
maradhi ya moyo nchini Tanzania kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika
zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ni mbili , moja ni homa ya Rumatiki pamojaa
na magonjwa ya moyo ya kurithi au kuzaliwa nayo .
Inaendelea
Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii , Dokta
SEIF RASHID amesema , huduma za upasuaji wa moyo katika Hopsitali ya Taifa
Muhimbili ilianza Mei 21 , 2008 na mpaka sasa huduma zinazopatikana ni za
upasuaji wa moyo , matibabu ya moyo , vipimo vya moyo na uchunguzi wa mishipa
na shinikizo.
Kwa mujibu wa Dokta SEIF RASHID
kutoka mwaka 2008 mpaka mwaka 2015 wagonjwa 600 wamefanyiwa upasuaji wa Moyo na hadi
kufikia Agosti mwaka huu Taasisi imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo 145
idadi hii inajumuisha wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo na waliozibwa matundu ya moyo
bila upasuaji.
Naye Mwenyekiti wa Bodi Hospitali ya
Taifa Muhimbili Profesa JOSEPH
KUZILWA amesema taasisi hiyo ni ya
kisasa , yenye vifaa vya hali ya juu vinavyotumia teknolojia ya kisasa katika
uchunguzi na tiba ya magonjwa ya moyo.
Akielezea mafanikio Profesa KUZILWA amesema
kwa kushirikia na Madaktari bingwa kutoka nchi rafiki ,kituo kimefanya upasuaji
wa moyo kwa wagonjwa 148 , kimechunguza mishipa ya moyo kwa kutumia kifaa
maalum kwa wagonjwa 160 , kimewawekea Stents wagonjwa 9 na kuwawekea vifaa vya
mapigo ya moyo wagonjwa 13.
Jengo hilo lenye thamani ya Shilingi
Bilioni 16. 6 limejengwa na Serikali ya China ambapo serikali ya Tanzania imenunua vifaa vyenye
thamani ya Shilingi Bilioni
No comments:
Post a Comment