Na Ally Daud –MAELEZO
Idadi ya mauzo katika soko
la hisa la Dar es salaam DSE limeshuka kwa asilimia 62 kutoka shilingi bilioni 6.4
hadi kufikia shilingi bilioni 2.4 ambapo zimeuzwa na kununuliwa katika soko zimeshuka
kutoka milioni 4.3 hadi kufikia milioni 2.7.
Akiongea na waandishi wa
habari Meneja Miradi na Biashara waDar es salaam Stock Exchange Bw. Patrick Mususa alisema kuwa hata hvyo idadi ya mtaji katika
soko umekuwa kutoka tilioni 21.9 hadi tilioni 22.3 ikiwa pia na idadi ya mtaji wa
makampuni ya ndani imekua tilioni 9.9.
AidhaBw. Mususa ameitaja
benki ya CRDB kuwa ndiyo imeongoza kwa kuuza hisa zake katika soko ikiwa na asilimia
92 ziki fuatiwa na Kampuni ya Swissport yenye asilimia 4 na Twiga Cement ambayo
ina asilimia 1.
“Kampuni ambazo zimeongoza
kwa ongezeko la bei katika soko la hisa ni Kenya Airways yenye asilimia 9 pamoja
na Kampuni ya bia ya East Africa Breweries ambayo ina asilimia 6 pamoja na Kampuni
ya uchimbaji wa madini ya Acacia yenye asilimia 3”,alisema Bw.Mususa.
Aidha Bw.Mususa aliendelea
kusema kuwa viashiria vya soko vimeshuka kwa alama 41 za huduma za kibenki kutokana
na kuongezeka bei ya hisa za CRDB kwa alama 3.7 ikifuatiwa na viwanda kwa alama
21 kutokana na ongezeko la bei ya hisa za TBL halikadhalika viashiria vya biashara
kuongezeka kwa zaidi ya alama 40 ikiwa imechangiwa na ongezeko la bei ya hisa ya za Kampuni ya Swissport kwa asilimia
0.13,kwa ujumla kiashiria cha soko kimeongezeka kwa asilimia 54.
Mbali na hayo Meneja Mradi
huyo alisema wameweza kuongeza wateja kwa kupitia huduma ya kimtandao ya DSE Mobile
Trading ambayo inawawezesha kujiunga ,kununua na kuuza hisa kupitia simu ya mkononi
kwa kupiga *150*36#.
No comments:
Post a Comment