Mkurugenzi
wa Elimu ya juu kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi,
Prof. Sylivia Temu (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na
uongozi wa chuoChuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha
Muhimbili (MUHAS), wawakilishi kutokakutoka Benki ya Maendeleo ya
Afrika (AfDB) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya baada
yauzinduzi
mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya
moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho
kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye
magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa
chini ya usimamizi wa (MUHAS).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS),
Prof Ephata Kaaya akizungumza wakati wa uzinduzi mradi wa ujenzi wa
kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini
uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho kitakachokuwa na
uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa
nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi
wa (MUHAS).
Muwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika Bw. Demissie Dejene akizungumza
wakati wa uzinduzi mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya
magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam
jana. Kituo hicho kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na
kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika
mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)
Na Mwandishi wetu,
SERIKALI
imezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na
mishipa ya moyo hapa nchini kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za
kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa
Afrika mashariki.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana
kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Bw. Shukuru
Kawambwa, Mkurugenzi wa Elimu ya juu nchini, Prof. Sylivia Temu alisema
mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa ushirikiano na benki ya
maendeleo ya Afrika ni
mojawapo ya miradi minne ya afya inayotekelezwa kwenye ukanda wa afrika
mashariki ikilenga kutatua changamoto mbalimbali za kiafya.
“Kila
nchi ya Afrika Mashariki ina mradi wa aina yake kwenye sekta hii muhimu
na kwa upande wetu sisi umejikita katika kukabiliana na magonjwa ya
moyo na utakuwa chini ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) na
utakwenda sambamba na ujenzi wa kampasi mpya ya chuo hicho unaondelea
huko eneo la Mloganzila hapa jijini Dar es Salaam,’’ alibainisha.
Akizungumzia
faida za mradi huo Prof Temu alisema utasaidia kupunguza vifo
vitokanavyo na magonjwa ya moyo hapa nchini sambamba na kupunguza
gharama zinazolikabili taifa kwa sasa kutokana na kusafirisha idadi
kubwa ya wagonjwa wa moyo kwa ajili ya kutafutaa matibabu nje ya nchi.
“Lakini
pia kupitia kituo hiki kitakacho kuwa kikubwa kabisa hapa Afrika
Mashariki tunarajia kwamba tafiti nyingi za masuala ya kiafya hasa
kwenye eneo hili la magonjwa ya moyo zitakuwa zikifanyika hapa nchini na
pia kupitia MUHAS tuzalisha wataalamu wengi wa magonjwa hayo kwa
manufaa ya vyuo vingine ndani na nje ya nchi,’’ aliongeza.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof Ephata Kaaya alisema
chuo chake kimejipanga kutekeleza mradi huo mkubwa utakaotekelezwa kwa
awamu mbili ambapo awamu ya kwanza utahusisha mafunzo pamoja na
maandalizi ya vifaa huku awamu ya pili ikuhusisha ujenzi kamili wa kituo
hicho.
“Tafsiri
ya uzinduzi huu ni kwamba MUHAS tunapewa heshima ya kusimamia kituo
hiki muhimu na kikubwa kabisa kwa Afrika masshariki na hakitahudumia
watanzania pekee bali nchi zote wanachama kutokana na ukweli kwamba na
nchi nyingine pia nazo zinaendesha miradi yenye hadhi kama hii ila
katika Nyanja tofauti za kiafya,’’ aliongeza
Akizungumza kwenye uzinduzi huo pia Meneja
Miradi ya Jamii kutoka benki ya Maendeleo ya Afrika Bw. Hamis Simba
alizitaja baadhi ya sababu zilisababisha benki hiyo kufadhiri mradi kuwa
ni pamoja na wao kuvutiwa na mikakati ya Tanzania na nchi za Afrika
Mashariki kwa ujumla katika kukabiliana na magonjwa ya moyo.
No comments:
Post a Comment