Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (kushoto) akizungumza na watumishi wa mashirika mbalimbali yaliyoko katika kambi ya Wakimbizi
ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma (hawapo pichani) wakati wa
ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil
(kulia) aliyetembelea kambi hiyo jana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abdulwakil (kulia), akizungumza na watumishi mbalimbali (hawapo pichani) wakati
wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo inahifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) na Burundi.
Daktari wa Hospitali ya Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Florence Mshana(aliyeshika
karatasi), akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mbarak Abdulwakil(kushoto), alipotembelea hospitali hiyo wakati wa ziara
yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma. Kambi hiyo inahifadhi wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Amah Assiama-Hillgartner( kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil(katikati), aliyetembelea hospitali hospitali hiyo wakati wa ziara yake katika
kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abdulwakil (katikati), akiongozana na Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B), Fredrick
Nisajile (kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi
(UNHCR) Ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa ziara ya
Katibu Mkuu kambini hapo jana. Kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma inahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) na Burundi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abdulwaki l(katikati), akiongozana na Mkuu wa Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu (B),
Fredrick Nisajile (kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa
ziara ya Katibu Mkuu katika makazi ya
wakimbizi yaliyopo Nyarugusu wilayani Kasulu
mkoani Kigoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abdulwakil, akimsikiliza mmoja wa maofisa wa Shirika la Chakula Duniani (WFP)
alipotembelea ndani ya mahema wanakoishi wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu
iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
PICHA ZOTE NA KITENGO
CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment