Ubao wa Matangazo ndani ya Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa, ukionyesha matokeo ya kura katika tukio la kihistoria
kufanyika ambapo Baraza hilo limepitisha azimio linalotoa fursa kwa
Palestina kupeperusha bendera yake. Nchi wanachama walipiga makofi
kushangilia kupitishwa kwa azimio hilo, ambalo Israel imesema Palestina
inatafuta umaarufu kwa njia za mkato badala ya kurejea kwenye meza ya
mazugumzo.
Na
Mwandishi Maalum New York
BARAZA
Kuu la Umoja wa Mataifa, jana Alhamis,
limepitisha Azimio ambalo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Umoja huo, litaruhusu
nchi ambazo siyo mwanachama kamili kupeperusha bendera yake katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Kupitishwa
kwa azimio hilo ambalo limepigiwa
kura za ndiyo 119 za hapana nane
na zisizofungamana na upande wowote 45 kunaipa fursa Palestina kupeperusha bendera yake nje ya Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa.
Mara
baada ya matokeo ya kura kutangazwa
rasmi, Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa walipiga makofi kama ishara ya
kufurahia kupitishwa kura nyingi azimio hilo.
Palestina kama ilivyo kwa Vatican inahadhi ya Nchi
Mwangalizi isiyo Mwanachama wa Umoja wa Mataifa (Non -Member Observer States)
Kwa
mujibu wa Azimio hilo nambaA/69/L.87
linaloelezwa kuwa ni la kihistoria,
linamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha
kwamba Bendera ya Palestina
inapeperushwa ndani ya siku 20 (
septemba 30)wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la
70 la Umoja wa Mataifa.
Akiwasilisha
azimio hilo mbele ya wajumbe, Mwakilishi wa Kudumu wa Iraq na ambaye ni mwenyekiti wa kundi la nchi
za kiarabu alisema kupeperushwa kwa
bendera ya Palestina ni kielelezo cha utekelezaji wa matakwa yaliyomo ndani
ya Katiba ya Umoja wa Mataifa ya kwamba,
nchi zote na watu wake wako sawa na wana haki
sawa.
Hata
hiyo si mataifa yote yaliyoridhika ya uamuzi huo, kwa kile ambacho wengine
wameeleza kuwa ni ukiukwaji wa kanuni za
Umoja wa Mataifa ambazo zinaeleza wazi wazi kwamba bendera zinazopashwa
kupeperushwa katika Umoja wa Mataifa ni
zile tu za nchi ambazo ni wanachama
kamili.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Kudumu wa
Israel katika Umoja wa Mataifa, yeye
alisema kwamba kupeperushwa kwa
bendera ya Paletina katika Umoja wa Mataifa, hakubadilishi hali halisi
na mazingira ya sintofahamu yanayoendelea kati yake na Palestina.
Akizungumza kwa hisia kali
huku akizilaumu nchi ambazo zimeunga mkono azimio hilo, Mwakilishi huyo
wa Israel, ameeleza kwamba Palestina inatakiwa kufanya maamuzi magumu yakiwamo
ya kurejea katika meza ya mazungumo
badala ya kutafuta njia za mkato
zikiwamo hizo za kupeperusha
bendera katika Umoja wa Mataifa.
Akasema yeye kama mwakilishi wa Israel picha ambayo
anaamini ndiyo inayostahili kuwa maarufu ni ile ya viongozi wa Israel na
Palestine watakapokuwa kwa pamoja wanapandisha bendera ya matumaini inayoonesha mataifa hayo mawili yakiishi kwa pamoja kwa Amani na usalama.
Hoja
ya kutaka Israel na Palestina kurejea
kwenye mazugungumo ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu baina ya pande hizo
mbili imeungwa mkono na wazungumzaji
wengi wakiwamo wale waliopiga waliopiga
kura ya hapana kama
vile Marekani .
Kwa upande wa wale waliounga mkono azimio hilo,
walieleza kwamba nchi inapo peperusha bendera yake hata ni kielelezo cha ufahari, utambulisho na
uwepo wake na kwa sababu hiyo Palestine ilikuwa na kila sababu ya kupeperusha bendera yake ambayo kwayo
haibadilishi hadhi yake ya kuwa nchi mwangalizi, lakini ikiandika historia
nyingine.
Mwakilishi
wa Palestina akiwa na furaha tele
amezishukuru nchi zote ambazo zimeunga mkono azimio hilo.
Pamoja
na kupitishwa kwa Azimio hilo linalotoa
fursa kwa nchi ambazo si wanachama kamili kupeperusha bendera,
Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa pia walipitisha kwa kupiga kura
azimio linalotaka kuangaliwa kwa misingi ya utaratibu wa marekebisho ya ulipaji wa madeni kwa nchi zinazodaiwa.
Azimio
hilo namba A/69/L.84 lililowasilishwa na Mwenyekiti wa Kundi la Nchi 77 na China (
G77&China) lilipita kuwa kura 136 za ndiyo, sita za hapa na 41 zisizofungamana na upande wowote
No comments:
Post a Comment