MFUMO WA KIMTANDAO UNAOWEZESHA
KUPOKEA NA KUHAMISHA MIAMALA YA KIFEDHA KUTOKA BENKI MOJA KWENDA NYINGINE
UNAORATIBIWA NA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT)
YAANI ‘TANZANIA INTER-BANK SETTLEMENT SYSTEM’ (TISS) WAONGEZA UFANISI
KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga, akibadilishana
mawazo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire, leo
asubuhi kabla Kaimu Katibu Mkuu hajaongea na waandishi wa habari pamoja na
wadau kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwa kuongeza muda malipo ya kibenki
kupitia mfumo wa TISS.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire (wa tatu kutoka kushoto),
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na wadau mbalimbali, kuhusu mafanikio
yaliyopatikana kwa kuongeza muda malipo ya kibenki kupitia mfumo wa TISS.
Wadau
mbalimbali wa Bandari ya Dar es Salaam na waandishi wa habari wakimsikiliza
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw Gabriel Migire (hayupo pichani)
wakati akieleza mafanikio yaliyopatikana
kwa kuongeza muda malipo ya kibenki kupitia mfumo wa TISS, leo asubuhi katika
ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA).
Mkurugenzi
wa mfumo wa malipo kitaifa wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw, Benard Dadi, akieleza
mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kuongeza muda wa malipo ya kibenki kupitia
mfumo wa TISS, leo asubuhi katika Ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA).
Mkurugenzi huyo ameziomba benki kukubali kupokea na kuhamisha malipo kupitia mtandao wa TISS kwa zaidi ya
muda wa awali wa ukomo ambao ulikuwa saa saba mchana.
Kamishna
wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Tiagi Kabisi, akieleza
namna mifumo mbalimbali inayotumiwa na Mamlaka ambayo imeunganishwa na Mfumo wa
TISS ilivyoongeza mapato na kurahisha huduma mbalimbali za malipo, leo asubuhi
katika Ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Uchukuzi)
No comments:
Post a Comment