Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza
na wananchi juu ya kutambua michango ya kimaendeleo inayofanywa na
wanawake kwa kuwawekea kumbukumbu kama ilivyo kwa wanaume, ili kuleta
uwiano wa kijinsia leo Jiji Dar es Salaam katika kilele cha tamasha la
Jinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akiteta jambo na Ruth Meena.
Wanawake wakitaja baadhi ya matatizo ambayo yanayowakabili ni pamaoja na suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama maeneo mbalimbali nchini.
Wanawake
wameitaka tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) kutofumbia macho suala la
matusi na kejeli zinazofanywa na viongozi wa siasa katika kampeni zao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akiwa
katika picha ya pamoja na wa mama walioshiriki maadhimisho hayo leo
jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wananchi waliofika katika maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam (Picha na Emmanuel Massaka).
WATANZANIA
wametakiwa kuchagua viongozi ambao sera ya ilani ya vyama vyao,
itatatua kero zao na iwe yenye kutekelezeka kwa mustakabali wa
maendeleo ya taifa na sio ya kibinafsi.
Wakiwakisilisha
maadhimio mbalimbali katika kilele cha Tamasha la Jinsia jijini Dar es
Salaam, wananchi kutoka warsha mbalimbali, wamesema kuwa watanzania
wametakiwa kuwa makini kwa kuwachagua viongozi ambao watawahaidi sera
zinazo tekelezeka na sio vinginevyo.
Wakitaja
baadhi ya matatizo ambayo yanawakabili ni pamaoja na suala la
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama maeneo mbalimbali nchini,
hivyo watahakikisha wanawauliza wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi
ikiwemo udiwani, ubunge na urais, ni kwa kiasi gani watashughulikia
suala la huduma ya maji.
Vilevile
wamesema chama kitakacho pata ridhaa ya kuiongoza Tanzania kwa awamu ya
tano, ifanye mabadiliko ya katiba ambayo yataondoa mfumo kandamizi
dhidi ya mwanamke, pia wameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kutofumbia macho suala la matusi na kejeli zinazofanywa na viongozi wa
siasa katika kampeni zao, jambo ambalo linaweza chochea uvunjifu wa
amani nchini, huku wakiwataka tume kutenda haki kwa vyama vyote vinavyo
shiriki katika uchaguzi mkuu.
Hivyo
wameitaka serikali kutambua michango ya kimaendeleo inayofanywa na
iliyofanywa na wanawake kwa kuwawekea kumbukumbu kama ilivyo kwa
wanaume, ili kuleta uwiano wa kijinsia, pia wamesema watahakikisha
wanaishauri serikali kuandaa sera maalumu itakayo tambua mchango wa
wanawake na kuweka kumbukumbu katika makumbusho maalum ya wanawake.
Huku
wakiwataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kwa kutoa elimu ya
uraia na masuala mbalimbali mtambuka yenye tija kwa maendeleo ya
ukombozi wa taifa.
Tamasha
hilo la kijinsia lililo andaliwa na wadau mbalimbali wa masuala ya
kijinsia kwa kushirikiana na mtandao wa kijinsia TGNP, limefikia kilele
leo jijini Dar es Salaam likibeba kauli mbiu ya mifumo kandamizi ya
Mageuzi ya mifumo kandamizi hayaepukiki.
No comments:
Post a Comment