Saturday, September 12, 2015

IDARA YA MIPANGO MIJI NA VIJIJI ZANZIBAR YAANDAA MRADI WA KUBORESHA MAENEO MATANO YA WAZI YA MJI WA ZANZIBAR CHINI YA UFADHILI WA SHIRIKA LA SDC LA SWITZERLAND.

 Mkuu wa Ushirikiano wa  Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzaania Romana Tedeschi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha maeneo matano ya wazi ya Mji wa Zanzibar kwa kuanzia na  Kiwanja cha Demokrasia Kibandamaiti utakaofadhiliwa na Shirika la SDC la nchi hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akizindua  Mradi wa kuboresha maeneo ya wazi ya Mjini  Zanzibar katika hafla iliyofanyika Idara ya Ardhi na Upimaji Forodhani Mjini Zanzibar, (kulia) Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Muhamad Juma
  Msaidizi  Fundi Mkuu wa Kampuni ya Ujenzi ya Landscape ya Switzerland Roland Raderschall akitoa maelezo ya  Mradi wa  mwanzo wa kuboresha  Kiwanja cha Demokrasia cha Kibandamaiti katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
 Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Zanzibar Muhamad Juma akitoa ufafanuzi kwa wananchi walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha eneo la wazi  la Kibandamaiti., (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Mgharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Ramani ya maeneo matano  ya wazi yatakayofanyiwa  uboreshaji  na Idara ya Mipango na Vijiji ambayo ni Kibandamaiti, Lumumba, Darajani, Chumbuni na Darajabovu. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments: