Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuzindua mradi wa uchimbaji Visima
vya Maji Zanzibar unaofadhiliwa na Mtawala wa RAS Al - Khaimah hpo Chumbuni.
Balozi Seif akishuhudi kasi ya maji inayotoka miongoni mwa Visima 50
vilivyochimbwa maeneo mbali mbali ya Zanzibar hapo Chumbuni ndani ya iliyokuwa
zamani studio ya Sauti ya Tanzania Zanzibar.
Balozi Seif akibadilishana
mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Rak Gas ya Ras Al-Khaimah Bwana Kamal Ataya aliyemuwakilisha Mtawala wa
Nchi hiyo katika uzinduzi wa Visima vya Maji hapo Chumbuni Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Rak Gas ya Ras Al-Khaimah Bwana Kamal
Ataya wa kwanza kulia akiambatana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif kwenda kukagua Tangi la kuhifadhia
maji lililojengwa ndani ya eneo la zamani la Studio ya Sauti ya Tanzania
Zanzibar Chumbuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maji Zanzibar Dr. Mustafa Garu aliyevaa kofia ya Buluu akimkaguza Balozi Seif
kwenye Tangi kubwa la kuhifadhi Maji Chumbuni.
Muonekano wa Tangi Kubwa la kuhifadhia
Maji safi na salama ujazo wa Lita Laki
200,000 katika eneo la Chumbuni Mjini Zanzibar.
Picha na –OMPR – ZNZ.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi ameagiza kuanzia sasa kila Mwananchi ana wajibu wa kutambua kwamba analo
jukumu la kulinda Vyanzo vya Maji katika maeneo wanayoishi ili visichafuliwe
kwa shughuli yoyote ile isiokuwa ya Mamlama ya Maji Zanzibar.
Alisema licha ya kwamba upatikanaji wa huduma za
Maji safi hapa Nchini sio mbaya, lakini Jamii inapaswa kuwa na tahadhari katika
matumizi ya huduma hiyo kwa vile ifikapo mwaka 2030 nusu ya watu Duniani kote watakabiliwa na upungufu wa Maji.
Akizindua Mradi wa Uchimbaji wa Visima Zanzibar
unaofadhiliwa na Serikali ya Ras Al-
Khaimah hapo studio ya zamani ya Sauti ya Tanzania Zanzibar Chumbuni Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hali ya upatikanaji wa
huduma ya maji katika kipindi hicho itakuwa mbaya zaidi katika Nchi za Kiafrika
hasa zile zilizomo ndani ya Janga la Sahara.
Balozi Seif Alisema kwamba maji ni muhimu kwa maisha
ya Viumbe hasa Binaadamu. Hivyo ni vyema wana jamii wanapaswa kukumbushana juu
ya umuhimu wa matumizi bora ya maji.
Alieleza
kwamba upotevu wa huduma ya maji katika
maeneo mengi hapa nchini haikubaliki hata kidogo jambo ambalo Serikali Kuu inatoa onyo kali kwa wahalifu wanaohusika
na tabia hiyo na watakapopatikana waakiharibu miundombinu ya Sekta hiyo watachukuliwa
hatua za Kisheria.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Chama cha
Afro Shirazi (ASP) na sasa Chama cha Mapinduzi ilikuwa ikitoa kipaumbele suala
la kuwapatia wananchi wake maji safi na salama mijini na vijijini.
Akitoa salamu za Mtawala wa Ras AL Khaimah Emir Saud Bin
Saqr Qasimi Mkurugenzi wa Kampuni ya Rak Gas Bwana Kamal Ataya aliipongeza
Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar kutokana na mashirikiano iliyotoa katika
kufanikisha mradi huo katika awamu ya kwanza.
Bwana Kamal aliahidi kwamba Serikali ya Ras Al Khaimah
kupitia Kampuni hiyo imeahidi kukamilisha kugharamia awamu ya pili ya Uchimbaji
wa Visima 50 vilivyobakia kutokana na Mkataba uliofungwa.
Mapema akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuuzindua mradi huo wa uchimnbaji Visima
Zanzibar Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Zanzibar Mh. Ramadhan
Abdullah Shaaban alisema kwamba Wizara hiyo inakusudia kuona tatizo la huduma
ya maji safi na salama hapa Nchini litabakia kuwa Historia.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment