Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akifungua Pazia kuashirika kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa
Nyumba ya Kuishi Askari Polisi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
Kaskazini Pemba.
Iddi akifungua Pazia kuashirika kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa
Nyumba ya Kuishi Askari Polisi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
Kaskazini Pemba.
Balozi Seif akikagua moja ya vyumba Kumi vilivyomo
ndani ya jengo linalojengwa kwa ajili ya makaazi ya Askari Polisi
Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
ndani ya jengo linalojengwa kwa ajili ya makaazi ya Askari Polisi
Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.
Baadhi ya Makamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Kaskazini Pemba wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani
ambapo wa kwanza kutoka kulia ni OCD Wilaya ya Micheweni Kamanda Haji Miraji na anayefuatia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba RPC Moh’d Shehani.

Baadhi ya Vijana wa Vikundi vya Polisi Jamii vya
sheria zilizomo ndani ya Wilaya ya Micheweni walijumuika katika hafla
ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba ya Askari wa Wilaya
hiyo ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif.

Balozi Seif akihutubia Makamanda, wapiganaji wa
Jeshi la Polizi na Vikundi vya Polisi Jamii mara baada ya kuweka Jiwe
la msingi la ujenzi wa nyumba ya Askari wa Wilaya ya Micheweni.
Jeshi la Polizi na Vikundi vya Polisi Jamii mara baada ya kuweka Jiwe
la msingi la ujenzi wa nyumba ya Askari wa Wilaya ya Micheweni.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Mh. Omar Khamis
Othman, Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna msaidizi wa Polisi Moh’d
Shehani na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Micheweni OCD Haji Miraji.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba
Heshima ya Jeshi la Polisi Nchini Tanzania itaendelea kuwepo endapo
ujenzi wa Nyumba za Makazi ya askari wa Jeshi hilo utaimarishwa na
kuendelezwa katika maeneo mbali mbali hapa Nchini.
Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akizungumza na Makamanda,
Askari wa Jeshi la Polisi, Vikundi vya Polisi jamii na Wananchi mbali
mbali mara baada ya kuweka Jiwe la msingi la Nyumba ya kuishi Askari
inayojengwa katika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema mfumo uliopo hivi sasa kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi
kuishi katika maeneo ya Kiraia unasababisha muhali kwa askari hao
wakati wanapolazimika kuchukuwa hatua za kisheria dhidi ya Watu
waofanya makosa ambao wanakuwa katika mazingira ya pamoja wakati
wote.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi wa Wilaya ya
Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba kupitia Vikundi vyao vya Ulinzi
Shirikishi na Polisi Jamii kwa uamuzi wao wa kushirikiana na Jeshi la
Polisi katika kuanzisha Ujenzi wa Nyumba hiyo ya kuishi Askari Polisi
Wilaya ya Micheweni.
Balozi Seif aliwaasa watendaji wa Jeshi la Polisi Nchini kuendelea
kusimamia sheria kikamilifu kwa kuzingatia maadili mema wakati wa
kutatua matatizo yanayoisumbua Jamii katika Maeneo yao.
Alisema ipo tabia ya baadhi ya askari wa Jeshi hilo kupendelea
kuwabeba watu maarufu,wenye uwezo na hata baadhi ya wageni wanaowekeza
vitega uchumi Nchini kwa kuzingatia kupata kitu kidogo jambo ambalo ni
kwenda kinyume na maadili yao ya kazi.
Katika kuunga mkono ujenzi huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif aliahidi kugharamia ukamilishaji wa vyumba vya kulala
Wageni katika Jengo hilo na kuuomba Uongozi wa Jeshi hilo kufanya
thathmini itakayomsaidia kuelewa gharama zitakazohitajika katika
kukamilisha vyumba hivyo.
Akitoa Taarifa ya Ujenzi wa Nyumba ya kuishi Askari wa Wilaya ya
Micheweni Kamanda wa Upelelezi na Makosa ya Jinai wa Wilaya ya
Micheweni Mkaguzi wa Polisi { Insector } Fakih Yussuf Mohammed
alisema mradi huo umekuja kutokana na ufinyu wa Makaazi uliokuwa
ukiwakumba askari wa Jeshi hilo kwa kipindi kirefu sasa.
Mkaguzi wa Polisi Fakih alisema matunda ya Falsafa ya Polisi Jamii
imeanza kutoa matunda kwa vile ujenzi wa nyumba hiyo ulioanza Mnamo
Tarehe 1 Septemba mwaka 2014 pia umeshirikisha wananchi wa shehia 27
zilizomo ndani ya Wilaya hiyo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanbzibar
6/9/2015.
No comments:
Post a Comment