Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisistiza jambo katika mkutano huo.
Wananchi
wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Jamhuti mjini Morogoro kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo Dkt Magufui aliwahutubia wananchi
hao sambamba na kuzinadi sera zake
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha
Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa
Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiwapungia
mikono wananchi huku wakiwa wameshika kofia zao.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
(CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubi maelfu ya wananchi kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa
Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.
Mmgombea
Urais Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.John Magufuli amesema iwapo
atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu mwaka huu ,Serikali yake
itashusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa bati na saruji. Dk.Magufuli
alitoa kauli hizo leo wakati anazungumza kwa nyakati tofauti katika
maeneo ya Mkamba.Ruaha.Mikumi,Kilosa mjini pamoja na Morogoro mjini
ikiwa ni sehemu ya kuomba ridhaa ya kuomba kichaguliwa urais katika
uchaguzi mkuu mwaka huu.
Alisema
kuwa serikali yake inataka kurahisisha maisha ya watanzania wote na
hivyo atapunguza bei saruji na bati na hilo litafanikiwa kwa kupunguza
ushuru wa vifaa hivyo."Serikali ya Magufuli nataka iwe ya kurahisisha
maisha ya wananchi wake.Moja ya mambo ambayo ninedhamiria kuyafanya ni
kupunguza bei ya bati na saruji.Nataka kuona watu wanajenga nyumba nzuri
na za kisasa, hivyo lazima tushushe bei ya vifaa vya ujenzi,alisema
Dk.Magufuli.
Aliongeza
kasi ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka hiyo anaiweza na anaomba
wananchi wamuamini na ameomba urais kwa ajili ya kufanya kazi tu huku
akieleza wapo ambao wanaosema anafanya siasa wajue yeye si
mwanasiasi.''Nataka kuwa Rais wa Tanzania na si uwenyekiti .Dhamira
yangu ni kuwatumikia watanzania kwa kuleta maendeleo yakiwemo ya kuwa na
makazi bora.
"Natambua
nchi yetu ni tajiri sana na sasa utajiri huo utumike kuleta maendeleo
ya wananchi na hili linawezekana kwenye serikali ya awamu ya tano,"
alisema Dk.Magufuli.Alisema rasilimali za nchi hii zitumike kuleta
maendeleo na ndio maana anataka nafasi hiyo kwa ajili ya kusimamia
maendeleo ya wananchi wote.Wakati huo huo,Dk.Magufuli aliwataka wananchi
kumchague yeye awe Rais kwa sababu hana tamaa ya fedha na ndio maana
amaweza kusimamia vema fedha za wafadhili ambazo zilitumika kwenye
ujenzi wa barabara.
Kwa
upande mwingine alisema atasimamia amani ya nchi kwani ndio msingi wa
maendeleo ya taifa letu na kuongeza shida ya watanzania si vyama vya
siasa bali ni maendeleo yao.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
(CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la
Morogoro mjini,Mh Azizi Abbod mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo
pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika
uwanja wa Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.
Mwenyekiti
wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akiteta jambo na Kada
maarufu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba jioni ya leo kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri mkoani Morogoro
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akizungumza
jambo na mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri
mkoani Morogoro.
Mwenyekiti
wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Kada
maarufu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba jioni ya leo kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri mkoani
Morogoro,pichani kati ni mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akishuhuhudia
tukio hilo.
Wananchi
wa kata ya Kimamba wakiwa wamekusanyka kwa wingi wakimsikiliza Dkt
Magufuli alipokuwa akijinadi kwao na kuomba ridhaa ya kuonza Tanzania
katika awamu ya Tano
Wanafuatilia
kwa makini maneno aliyokuwa akiyazungumza Mgombea Urais wa CCM Dkt John
Pombe Magufuli wilayani Kilombero mapema leo mchana.
Wananchi wa Luaha wilayani Kilombero wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hdahara
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Mikumi Ndugu Jonas Estomih Nkya.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mlimba Bw.Godwin Emmanuel Kunambi.
Wakazi
wa Mikumi wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowasili
maeneo hayo alipokuwa akielekea wilayani Kilosa kuhutubia mkutano wa
hadhara.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akifurahia jambo na mmto mara naada ya
kumaliza mkutano wa hadhara katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo.
Maelfu ya wananchi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wasanii
wa Bongo MOvie nao walikuwepo wakiongozwa na Steve Nyerere na Wema
sepetu katika kutimiza kampeni yao ya Mama ongea na Mwanao
Wapiganaji kazini
Kundi la Wasanii wa Filamu nchini la Mama Ongea na Mwanao likitumbuiza katika mkutano huo.
Wema Sepetu akizungumza jambo
Nyomi la Watu
No comments:
Post a Comment