Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Rais Sazi Salula akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu
Miradi ya majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu
(MKUHUMI) leo jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa wawezeshaji
kutoka Asasi isiyo ya kiserikali ya Niras kutoka Finland inayosimamia Miradi ya
majaribio nchini wa Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) Merja
Makela akitoa mada wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya
kuhifadhi mazingira na kuboresha usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka
kwenye misitu. Mkutano huo ambao umefanyika leo jijini Dar es salaam
umeandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Norway.
Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Rais Sazi Salula (kushoto) akifuatilia mada wakati wa mkutano wa
wadau wa mazingira kuhusu namna bora ya kuhifadhi mazingira na kuboresha
usimamizi wa ardhi na kuongeza mapato kutoka kwenye misitu. Wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu.
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu Miradi ya majaribio wa
Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) nchini wakifuatilia mada
wakati wa mkutano leo jijini Dar es salaam.
Mhadhiri kutoka
chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Pius Yanda akibadilishana mawazo na
Mwakilishi wa Ubalozi wa Ufaransa mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa
mazingira leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa
Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu (aliyevaa suti
nyeusi) akiongea na baadhi ya waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa mkutano
wa wadau wa mazingira leo jijini Dar es salaam.
Picha na Eleuteri
Mangi-MAELEZO)
Na Jenikisa
Ndile-MAELEZO
Watanzania wameaswa
kuzingatia namna bora ya kuhifadhi mazingira, upangaji wa matumizi bora ya
ardhi na utekelezaji wa mipango ili kuleta tija na maendeleo endelevu nchini.
Kauli hiyo imetolewa na
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula leo jijini Dar es salaam
alipokuwa akifungua Mkutano wa wadau wa mazingira unaohusu utekelezaji wa
miradi ya majaribio ya Mkakati wa Kupunguza Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI)
nchini.
Bw. Sazi alisema kuwa
mipango hiyo ya MKUHUMI inalengo la kuondoa umasikini kwa watanzania waishio
vijijini ambao wapo karibu na hifadhi za misitu
inasimamiwa na kutekelezwa kwa kushirikiana na Serikari ya kijiji ili
kuhakikisha mafanikio yanapatikana kwa kuzingatia utekelezaji na usimamizi wa
sheria kupitia kamati za vijiji.
Majaribio ya sera ya
mazingira yamefadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya
Norway ili kuboresha na kushughulikia masuwala ya ardhi, misitu na kupunguza
gesi joto kwa kuhimiza jamii kupanda miti kwa shughuli za maendeleo endelevu
nchini.
Mipango hiyo
inatekelezwa katika wilaya za Sumbawanga, Lindi, Kilwa, Zanzibar, Pemba, Kigoma
na Kondoa ambapo sera hiyo imewapa elimu ya kujenga utayari wa shughuli za
MKUHUMA na kuwezesha ushiriki mpana wa wadau ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake
Kiongozi wa miradi ya majaribio ya MKUHUMI Merja Makela alisema kuwa taasisi
yake imefanikiwa kutokana na kusimamia miradi hiyo ambayo imepokelewa na
kutekelezwa kama ilivyopangwa katika maeneo husika nchini.
Naye Mkurugenzi wa
Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu alisema kuwa kwa
tathmini iliyofanyika mwaka 2013, asilimia 55 ya ardhi ya Tanzania imefunukwa
na misitu ambapo juhudi zinaendelea kufanyika kwa kuwaelimisha watanzania
kuendelea kuitunza misitu hiyo kwa manufaa ya sasa na baadaye.
1 comment:
Post a Comment