Tuesday, August 11, 2015

MENEJIMENTI YA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA YAMPONGEZA MKUU WA MKOA HUO ENG. STELLA MANYANYA KWA USHINDI WA KISHINDO KURA ZA MAONI CCM JIMBO LA MBINGA MAGHARIBI

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma kwa ushindi mnono alioupata katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kutafuta mgombea wa ubunge Jimbo la Mbinga Magharibi. Eng. Manyanya alishinda kwa kura 13,276 ambapo mshindi wa pili alikua na kura 3,466. Jumla ya wagombea walikua 10 ambapo tisa kati yao walikuwa ni wanaume.

 Awali Jimbo hilo lilikuwa nimeshikiliwa na hayati Capt. John Komba. Kwasasa imebaki hatua ya mwisho ya majina ya wagombea kupitishwa na Uongozi wa juu wa Chama kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama  cha Mapinduzi majimboni katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2015. Uongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa unamtakia kila la heri Eng. Manyanya katika safari yake hiyo na hatimae aweze kushinda katika Jimbo hilo. 

Akitoa shukurani kwa niaba ya watumishi Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa kwa msukumo mkubwa wa maendeleo aliouweka katika kipindi cha uongozi wake hususani katika sekta ya elimu ambapo alianzisha Azimio la Kasense kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni, Kuboresha afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, usafi wa mazingira ambapo alianzisha kampeni ya Sumbawanga Ng'ara iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais, Kampeni ya upandaji miti, kuboresha mazingira ya utalii katika maporomoko ya Mto Kalambo, kuboresha hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa, Kuwaunganisha watumishi na viongozi katika kufanya kazi kwa pamoja n.k 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa katika kikao kifupi cha kumpongeza baada ya kushinda katika kura za maoni Jimbo la Nyasa Magharibi kupitia CCM. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Viongozi hao pamoja na watumishi kusimamia misingi aliyoiweka ya kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa, kufanya kazi kwa pamoja (team work) na kutekeleza majumu yao ya kila siku kwa ufanisi na ubunifu wa hali ya juu. Alisistiza kuwa maendeleo ya taifa la Tanzania hayataletwa tu kwa kutegemea vyama vya siasa bali kwa wananchi na wafanyakazi kutekeleza majukumu na wajibu wao ipasavyo kwa kuweka uzalendo mbele na kufanya kazi kwa bidii na uadilifu uliotukuka.   
 
 Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya akitoa Shukrani na Salamu za pongezi kwa niaba ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya kufuatia ushindi alioupata katika kura za maoni kutafuta mgombea wa CCM Jimbo la Mbinga Magharibi. Kwa sasa Mhe. Eng. Manyanya.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.

No comments: