Friday, August 7, 2015

UTUMISHI YAKABIDHIWA ZAWADI YA USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA YALIYOFANYIKA CONGO BRAZAVILLE

Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (katikati) akipokea cheti cha ushiriki wa Tanzania kutoka kwa Mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma  Barani Afrika Bw. William Budoya yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Florence Temba (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akipokea zawadi ya Tanzania kutoka kwa mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika Bw. William Budoya yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (katikati) akionyesha cheti cha ushiriki wa Tanzania katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni.  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Florence Temba (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (wa pili kutoka kushoto),  Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia) na mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo kutoka Wizara ya Uchukuzi Bw. William Budoya (wa kwanza kulia).

No comments: