Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani )juu ya kungatuka katika chama hicho na kujiunga na Chadema leo katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Kulia ni John Gudinita.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, John Gudinita akitangaza kujiuzuru katika chama hicho na Kujiunga na Chadema leo majira ya saa tano katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. kushoto Sheik Rajab Katimba na kulia ni Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.
Aliyekuwa.Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja akionesha kuwa yeye ni chandema kwa sasa.
Wandishi wa habari
wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja wakati akitangaza
kujiuzuru katika chama hicho na Kujiunga na Chadema leo majira ya saa tano
katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Na Chalila
Kibuda,Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja amengatuka uanachama
wa CCM pamoja kujiuzuru nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es
Salaam,Mgeja amesema kuwa ametafakari sana na kuona aungane na chama hicho.
Mgeja amesema kuwa
anaondoka kwenda kutafuta mabadiliko katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) na kuongeza kuwa wametumikia chama hicho kwa muda mrefu lakini sasa
imefika wakati wa kuondoka.
Aidha amesema kuwa CCM
ya sasa imekuwa na vitu ambavyo vinafanywa na watu baadaye kuikigharimu chama
kutokana na kuacha msingi wa kukubali maoni ya wanachama.
Wakati huo huo katika
mkutano huo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,John Guninita
naye amengatuka katika chama hicho na kujiunga ba Chadema kuongeza nguvu
Ukawa.
Guniinita amesema kuwa
sasa umefika wakati wa kuondoka kutokana na Chama kuacha kusikiliza wanachama
wake na badala yake kuendeleza chuki ndani ya Chama.
No comments:
Post a Comment