Waziri wa Kazi Viwanda na Ustawi wa Jamii wa Sierra Leone Dk. Methew Teambo na wawakilishi
wa mamlaka za afya kutoka nchini Sierra Leone wakiambatana na maasifa wa mfuko
wa bima ya afya Tanzania (NHIF) wemefanya ziara ya mafunzo katika hospitali ya
Kairuki iliyopo Mikocheni jijini, Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo ya mafunzo wameweza kuona utaratibu wa
Kairuki Hospital wa jinsi wanavyowahudumia wateja wa NHIF ambapo waziri na
wawakilishi kutoka Sierra Leone walikuwa na lengo la kuja kujifunza.
Pamoja na kupata mafunzo hayo, pia waziri na wawakilishi
wake wameweza kutembelea sehemu mbali mbali na kujione vifaa vya kisasa
vilivyopo katika hospitali hiyo. Akizungumza baada ya ziara hiyo, waziri
amesema “utaratibu huu wa NHIF ni mzuri kwani unashirikiana na sekta binafsi
katika kuwapatia huduma za afya wanachama na wananchi kwa ujumla”.
Hata hivyo, waziri amemshukuru Mkurugenzi wa hospital
hiyo Dr Asser Mchomvu kwa kukubali kuwapatia mafunzo hayo na kuapatia maelezo ya kina ya jinsi NHIF ilivyosaidia kutoa mwanga kwa namna mbali mbali kwa vituo
vya afya kuweza kufanyakazi na mfuko huo
katika kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko huo.
Waziri wa Kazi Viwanda na Ustawi wa Jamii wa Sierra Leone Dk. Methew Teambo akiwa Ndani ya chumba cha CT SCAN machine ya kisasa inayotumika kuchunguza maradhi mbalimbali ya binadamu alipotembelea Hospitali ya Kairuki.
Waziri akipiga picha kwenye chumba cha mammography Mashine ya kuchunguza saratani ya matiti (Mammography)
Wajumbe wa Management ya Kairuki hospitali wakizungmza na wageni to Sierra Leone.
Ujumbe toka Sierra Leone.
Dr Asser Mchomvu, Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki akimwonyesha waziri na ujumbe wake jinsi mat dal na mfumo wa computer hospitalini (eHSM) hapo unavyorahisisha katika kutoa huduma wa wagonjwa. MFumo huu ilianza tumika kwa mara ya Kwani nchini hapo Kairuki hospital.
Wageni wakionyesha mfumo wa huo.
Dk. Clementina Kairuki Nfuka ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu akitoa maelezo kwa Waziri na ujumbe wake.
Waziri wa Kazi Viwanda na Ustawi wa Jamii wa Sierra Leone Dk. Methew Teambo akiwa na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Management ya Kairuki Hospitali.
No comments:
Post a Comment