Moja kati ya changamoto tunayokutana nayo hapa Dudumizi pindi tunapofanya kazi za wateja wetu ni kuwa, wengi wao wamekuwa wakitaka kukamilisha kazi ya kesho leo.
Hii ina maana, mteja anataka website ambayo ina vitu vingi ambayo si lazima vyote vikamilike kwa siku moja.
Kwenye biashara yoyote, kama alivyoandika Simon Sinek's kwenye kitabu chake cha anza na kwanini, "Start with why" kuwa unatakiwa kuanza na sababu ya kuwepo kwa biashara yako, na si nini unatakiwa kufanya.
Kwa kujua hili, kutakusaidia kujua na kupanga hatua kwa hatua cha nini kifanyike kwenye muda gani ili kukidhi mahitaji ya wateja.
Ukiangalia website nyingi maarufu duniani kama Facebook, Twitter, Apple, Google, YouTube, eBay, LinkedIn, Yahoo, na Flickr zimekuwa zikibadilika kuendana na matakwa ya watumiaji na wakati. Hii ni kwa sababu, uwepo wao kwenye biashara unategemeana sana na mambo hayo muhimu. Kumbuka, hazina(muda na pesa) zina kikomo hivyo lazima kuwe na mpango endelevu.
Ni lazima uhakikishe unaweka mpango endelevu maboresho ya biashara yako (Continual Service Improvement), pia una malengo yaliyo moja kwa moja na njia thabiti ya kuyafikia. Website kama sehemu ya mpango huo, nayo inatakiwa kuwa inabadilika ili kuendana nayo.
Mfano, leo hii kuna Website nyingi sana Tanzania bado zina muonekano na mfumo wa miaka kumi iliyopita wakati ambao matumizi ya simu za mkononi hayakuwa makubwa.
Hata sasa, bado tumekuwa tukitumia muda mwingi kuwashauri baadhi ya wateja wetu wanaotaka kutengeneza website mpya kuachana na mifumo ya kizamani, kuna wengine hukataa katakata.
Leo, kwenye kila watu kumi, angalau sita wanatumia simu kufungua Website, hivyo ni dhahiri utahitaji website inayoendana na vifaa tofauti (responsive website), iwe ni simu, kompyuta mpakatoau hata tablet. Ukiwa na webite inayofunguka tu kwenye simu, ni dhahiri kuwa utapoteza wateja wengi.
Na kama bado hauna Website, jua kuwa muda si mrefu utakuwa nje wa uwanja wa ushindani. Hii ni kwa sababu, jinsi siku zinavyoenda, ndivyo mambo yanavyobadilika. Leo hii, mtu akihitaji huduma ya Website Design, anaenda tuu Google na kuandika Website Design In Tanzania, matokeo yatatokea na kuchagua walio bora na kuwasiliana nao, hapa huduma za uboreshaji wa matokeo ya utafutaji (Search Engine optimization) yanakuja.
Hivyo basi, hakikisha unamiliki Website yenye vigezo na unaiboresha siku hadi siku. Usiogope kuingia sokoni kwa kuwa na Website ya kawaida kwani hata Roma haikujengwa siku moja.Ila lazima uwe na mpango kazi endelevu unaotekelezeka.
Dudumizi tunayo package kwa ajili ya wajasiriamali kama wewe, tutumie maombi ( Ask for Quotation), hautojutia maamuzi yako.
No comments:
Post a Comment