Mratibu
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro
Rodriguez.
UMOJA
wa Mataifa umetaka vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa
kuhakikisha vinatoa taarifa zao kwa usahihi kuhusu maandalizi ya
uchaguzi na uchaguzi wenyewe.
Kauli
hiyo imetolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa Dar es salaam, kufuatia
taarifa iliyochapishwa na jarida moja kwamba UN inataka kujitoa katika
kusaidia mandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania.
Aidha
alisema kwamba si kweli kuwa Umoja wa Mataifa haujaridhishwa na
mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania na kwamba Umoja huo
utaendelea kushirikiana na serikali na vyombo vingine vya uchaguzi
kuhakikisha uchaguzi unakwenda vyema.
Indian
Ocean Newsletter ya Julai 10 mwaka huu ilichapisha habari iliyoandikwa
na kichwa cha habari “State is facing electoral commissions negligence”
na kusema kwamba Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
Tanzania na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, haridhishwi na mwenendo wa
maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe na kutishia kuondoa msaada wa
mamilioni unaoratibiwa na UNDP kutoka kwa wahisani mbalimbali.
Aidha Julai 15, 2015, mtandao wa Jamii Forum ilitafsiri habari hiyo kwa Kiswahili na kuitawanya kwa wasomaji wake.
Taarifa ambayo sio sahihi iliyochapwa na Jamii forum hii hapa link: http://www.jamiiforums.com/ jukwaa-la-siasa/885659-un- yaeleza-kutoridhishwa-kwake- na-vurugu-za-uchaguzi-nchini- tanzania.html#post13289399
Ukweli ulivyo
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini hajawahi kukutana wala kuzungumza na watu wa Indian Ocean Newsletter .
Aidha
taarifa zilizotolewa na kijarida hicho na tafsiri yake iliyowekwa
mtandao wa kijamii wa Jamii Forums hazikujengwa katika ukweli.
Pia
Umoja wa Mataifa utaendelea kufanyakazi na mamlaka za Tanzania na
wananchi wake na kuwa Uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na mamlaka za
uchaguzi nchini Tanzania na Jumuiya ya kimataifa inayofadhili mradi wa
DEP unawasilisha mahusiano muhimu miongoni mwa wadau mbalimbali
wanaotaka kuwapo na uchaguzi huru na wa amani.
Alisema
katika makubaliano kuna kamati ya mradi inayojumuisha wadau wote na ina
wajibu kuongoza na kutoa mwongozo wa utekelezaji mradi huo kimkakati.
Maamuzi ya mradi huo hufanywa na kamati hiyo na kamati ya ufundi ya mradi iliyopo Bara na Zanzibar.
Kutokana
na ukweli huo Umoja wa Mataifa unavitaka vyombo vya habari vya kitaifa
na Kimataifa kuhakikisha kwamba inatoa taarifa za ukweli na za usahihi
kipindi hiki cha maandalizi na uchaguzi wenyewe.
Biometric Voter Registration (BVR) Machines operator, Kheri Mkali
attends Rebeca Kimu at Bunju A in Dar es Salaam yesterday during the
trial registration. (LIBRARY PHOTO|VENANCE NESTORY).
Background
The
Democratic Empowerment Project is a three year project launched on the
12th of March 2013 and is directly executed by UNDP with UN Women and
UNESCO through a donor basket fund. It follows two previous electoral
support projects in Tanzania: the Electoral Assistance Project of 2005
and the Election Support Project of 2010. The USD 25m project has four
main components, namely, a) supporting legal and institutional reforms;
b) support improvement of Electoral Management body’s capacities(NEC and
ZEC); c) promote inclusive participation in political and electoral
processes, and d) support national peace infrastructures. More
specifically, the project has been supporting both NEC and ZEC to
improve their institutional capacity both in the context of the conduct
of the voter registration process (but not the provision of the BVR kits
which is the government’s responsibility) and the preparations for the
2015 general elections. DEP’s support has included technical and
advisory services, staff training, voter education and stakeholder
engagement. Such stakeholders include the Office of the Registrar of
Political Parties, political parties, media, civil society and groups
representing women, youth and people with disabilities. So far DEP has
supported and implemented most of these activities either directly or
via cooperation agreements with the electoral management bodies who
execute specific activities directly in line with their mandate.
Issued by: The Office of the UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative – Mr. Alvaro Rodriguez
For more information, please contactHoyce Temu-UN Communications Specialist at hoyce.temu@one.un.org or Aine Mushi, UN Coordination Specialist at aine.mushi@one.un.org
Below is the Indian Newsletter article in French
No comments:
Post a Comment