Thursday, July 23, 2015

FASTJET KUZINDUA SAFARI YA LILONGWE-MALAWI JULAI 27 MWAKA HUU

DSC_0263Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa habari akielezea kampuni hiyo ilivyoweza kusaidia sanaa kwa Tanzania na Afrika. Kushoto kwake ni CEO wa ZIFF, Prof. Martin Mhando.
Na Andrew Chale.
Shirika la ndege la Fastjet limeendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha ‘rout’ zaidi za safari zake ikiwa ni kuunganisha Afrika kuwa moja.

Kwa mujibu wa Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro anasema kampuni hiyo inatarajia kuizindua rasmi safari zake kwa kwenda, Malawi.
“Julai 27, Fastjet tutazindua rasmi safari ya kutoka Dar es Salaam-Lilongwe Malawi. Hii inakuwa ni ‘rout’ yetu ya tano katika safari zetu za Kimataifa ndani ya Afrika lengo ni kufikia nchi mbalimbali za Afrika.” Anabainisha Lucy Mbogolo.

Hata hivyo anabainisha kuwa, wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wateja wao juu ya huduma ya Fastjet Ambayo imeendelea kuwa bora zaidi kila kukicha huku akisisitiza kwa wateja kufanya ‘booking’ mapema pamoja na kuzielewa sheria na taratibu za usafirishaji wa anga.

Awali Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘rout’ za Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar sasa hivi wamevuka mipaka zaidi kwa nchi za Afrika zikiwemo, kati ya Dar – Johannesburg, Dar – Lusaka, Dar – Harare,Dar – Entebbe nah ii inayotarajiwa kuzinduliwa wiki ijayo ya Dar-Lilongwe.

Aidha, Lucy Mbogoro alibainisha kuwa Fastjet itaendelea kusaidia kukuza sekta ya sanaa nchini na Bara la Afrika kwa kuwaunganisha wadau wa sekta hiyo ikiwemo wasanii wa filamu, muziki na sanaa kwa ujumla.

Lucy Mbogoro anasema hayo ambaapo kwa mwaka huu ni mwaka wa pili mfululizo wakiendelea kudhamini tamasha la Filamu za nchi za majahazi maalufu kama ZIFF. DSC_0311Mwanamuziki wa Kimataifa, Moussa Diallo kutoka Mali (kushoto), akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa habari. Kulia kwake ni Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro ambao wamedhamini tamasha hilo kwa mwaka wa pili mfululizo kwa upande wa usafirishaji.. DSC_0328Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro akizungumza na waandishi wa habarimuda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo.. (Picha zote na Andrew Chale.)fastjetmoja ya ndege za Fastjet kama inavyoonekana pichani.

No comments: