Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akimpokea muigizaji maarufu wa filamu wa nchini Afrka Kusini,Jacky Devnarain maarufu kama Rajesh Kumar ,jina alilotumia katika tamthiliya ya Isidingo the Need aliposhuka yeye na wenzie 37 waliopanda mlima huo kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wasichana wanaotoka katika familia maskini.
Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya akimpatia kinywaji ,Muigizaji Jacky mara baada ya kufika katika lango la Marangu ,akishuka kutoka Mlima Kilimanjaro.
Muigizaji Jacky akisalimiana na Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Tanzania (TANAPA)Ibrahim Musa baada ya kushuka kutoka Kilele cha Uhuru ambako kati ya watu 37 waliopanda mlima huo ,32 ndio waliofanikiwa kufika kileleni.
Mkuu wa wiaya ya Siha ,Dkt Charles Mlingwa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya mapokezi ya ugeni huo ulioanda mlima Kilimanjaro akimkaribisha keki Muigizaji Jacky mara baada ya kuteremka kutoka Mlima Kilimanjaro.
Washiriki wa timu hiyo iliyopanda mlima Kilimanjaro kwa uratibu wa Mfuko wa Mandela wakifika katika lango la Marangu mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro.
Miongoni mwa wapandaji hao alikuwemo Ofisa Uhusiano wa nje wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom,Maya Makanjee.
Makanjee akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wenzake wa zoezi hilo mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro.
Washiriki wa zoezi hilo wakifurahia Keki iliyopambwa kwa rangi za Bendera ya taifa la Afrika Kusini,na Baba wa taifa hilo,Mzee Nelson Mandela akisalimia.
Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ,Erastus Runguro akizungumza jambo na muigizaji ,Jacky Devnarain (Rajesh Kumar).
Muigizaji Jacky akisindikizwa na Mhifadhi ,Charles Ngendo kupata sehemu ya kupumzika kwa muda .
Muigizaji Jacky(Rajesh Kumar ) akiwa amepumzika katika eneo maalumu la wageni
Muigizaji Jacky (Rajesh Kumar ) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Tanzania,Ibrahim Musa ,
Keki maalumu iliyotengenezwa na kupambwa kwa rangi za Bendera ya Taifa la Afrika Kusini iliyokabidhiwa kwa washiriki wa zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya familia maskini.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment