Mapema wiki iliyopita Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilitembelea miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini ili kukagua utekelezaji wake. Miradi hiyo ni pamoja na Kituo cha kuzalisha samaki Morogoro, Skimu ya Umwagiliaji Iringa vijijini, Maghala ya COWABAMA Iringa Vijijini, Ujenzi wa Barabara ya Iringa – Dodoma, Bwawa la Mtera, Ujenzi wa Barabara ya Manyoni – Itigi, utandikaji wa Reli eneo kati ya Kitaraka na Malongwe, Shamba la Kitengule, One Stop Border Post Mutukula, Mkongo wa Taifa Mutukula na Upanuzi wa mradi wa maji safi, Bomba Kuu la Ziwa Victoria.
Katika kufanikisha uratibu wa miradi ya maendeleo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango hufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzielekeza Wizara zinazotekeleza miradi kuwasilisha taarifa za utekelezaji kila robo mwaka. Aidha, Tume ya Mipango hutembelea miradi ya maendeleo kuona hali halisi ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kubaini mafanikio na changamoto na hatimaye kutoa ushauri katika ngazi husika kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Moja ya Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ni kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Kitaifa ya Kimkakati, Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (MMS) na miradi mingine muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa. Miradi imeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) na ile ya Matokeo Makubwa Sasa iliyoibuliwa katika mfumo wa kimaabara.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (wa nne kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa kwanza kushoto) na maafisa kutoka kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pamoja na wataalam wa Mradi wa Kituo cha Kuzalisha Samaki kilichopo Kingolwira Mkoani Morogoro wakiangalia sehemu maalum ya kukuzia vifaranga vya samaki baada ya kutotoleshwa.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma, hatua ulipofikia na changamoto zilizopo kutoka kwa Mtaalamu Elekezi wa mradi Bw.Robin de Kock (mwenye kofia).
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri (wa tatu kulia) akiangalia kazi ya ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma inavyoendelea wakati alipotembelea mradi huo pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Pamoja nao ni Mtaalamu Elekezi wa mradi Bw.Robin de Kock (mwenye kofia katikati).
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa pili kushoto) pamoja na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipewa maelezo kuhusu bwawa la kuzalisha umeme la Mtera kutoka kwa Meneja wa Kituo Bw. Abdallah Ikwasa (wa nne kushoto). Hii ni sehemu ambapo uzalishaji wa umeme unafanyika. Bwawa la Mtera linapatikana katika mikoa ya Iringa na Dodoma. Lina uwezo wa kuzalisha MW 80 ambao unaoingizwa katika Gridi ya Taifa.
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (wa kwanza kushoto) na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa reli kutoka Kitaraka hadi Malongwe mkoani Tabora kutoka kwa Bw. Raphael Mwandumbya (mwenye kofia) ambaye ni Mkaguzi wa ujenzi wa reli hiyo. Mradi huu ni sehemu ya ujenzi na ukarabati unaoendelea katika Reli ya kati ambao una urefu wa kilometa 89.
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa kwanza kushoto) na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiangalia uharibifu wa barabara ambao unafanywa na wananchi wasio waaminifu kwa kuchota kokoto pembezoni mwa barabara hiyo ambayo bado inaendelea kujengwa. Barabara hii inajengwa na Nicholas O’Dwyer & company Ltd Consulting Engineers ambapo kipande cha Manyoni hadi Itigi kipo katika hatua za mwisho kukamilika. Lengo la mradi ni kuendelea kujenga barabara ya Manyoni – Itigi kwa kiwango cha lami katika sehemu tatu za utekelezaji ambazo ni: Manyoni – Itigi – Chaya (KM 89.35), Chaya - Nyahua (KM 90), na Nyahua – Tabora (KM 85).
Jengo kwa ajili ya kutolea huduma za mpakani (One Stop Border Post) Mtukula, mradi ambao unahusisha ujenzi wa miundombinu inayosaidia utolewaji wa huduma bora na za kisasa mpakani mwa Tanzania na Uganda. Lengo la mradi wa One Stop Border Post ni kukamisha vituo vya utoaji huduma za pamoja mipakani kati ya Tanzania na nchi za jirani.
Timu ya maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (wa tatu kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa wataalam wanaohusika na Mkongo wa Taifa. Lengo la mradi kwa mwaka 2014/2015 ni mapitio ya miundombinu ya Mkongo na mifumo kwa ajili ya maboresho, ujenzi Awamu ya III sehemu ya kwanza ya upanuzi wa mkongo kwa maeneo yaliyobaki katika awamu I na II na uhakiki wa ubora wa Mkongo.
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omary Abdallah (wa kwanza kulia) na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kuhusu mafanikio na changamoto za Mradi wa Ranchi ya Taifa Misenyi kutoka kwa Meneja wa Mradi Bw. Martin Ladislaus (katikati). Shamba hili la mifugo lipo Karagwe, mkoa wa Kagera. Ni moja kati ya mashamba makubwa 9 nchini ya uwekezaji, limepimwa na kupata hati miliki.
Ujumbe kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ukiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (mwenye t’shirt nyeusi) wakiangalia sehemu ya kuogeshea ng’ombe. Wengine ni Meneja wa Mradi Ranchi ya Taifa Misenyi, Kagera Bw. Martin Ladislaus (wa tatu kulia) na Meneja wa Mradi Ranchi ya Kitengule, Kagera Bw. Hemedi M. Seif (wa pili kulia).
No comments:
Post a Comment