Wednesday, July 15, 2015

HUAWEI WAZINDUA SIMU MPYA AINA YA HUAWEI P8

 Meneja  Mkazi wa kampuni  ya Simu za mkononi,  Peter  Zhang akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu  uzinduzi wa simu mpya ya kisasa ya Huawei P8 katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regence  leo Jiji Dar es Salaam.
 Mkurungenzi wa Masoko  wa Huawei Tanzania Mamson Mjwala  akizungumza juu ya ubora wa betri ya simu hiyo aina ya Huawei P8 kwamba mfumo wa simu imezingatia matumizi ya muda mrefu mtumiaji anaweza kutumia simu kwa  siku nzima bila kuiongezea umeme huku kwa wale watumiaji wa kawaida anaweza kutumia kwa siku moja na nusu.
Meneja  Mkazi wa kampuni  ya Simu za mkononi, Peter  Zhang wa kulia  wakizinduwa simu hiyo ya Huawei P8 kushoto ni Mkurungenzi wa Masoko  wa Huawei Tanzania, Mamson Mjwala  wakionyesha simu hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regence leo Jiji Dar es Salaam
 Wadau wa simu aina ya Huawei huwafurahia simu hiyo Huawei P8 katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regence leo Jiji Dar es Salaam.
 Baadhi ya wapiga picha wakipiga picha za uzinduzi wa Simu ya Huawei.
Mkurungenzi wa Masoko  wa Huawei Tanzania, Mamson Mjwala  kimwonyesha simu ya Huawei mwandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regence leo Jiji Dar es Salaam.
PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

No comments: